1. Maana
Kitanzi ni kifaa kidogo cha plastiiki chenye vinyuzi mwishoni ambacho huwekwa kwenye mji wa mimba kupitia uke. Nyuzi zinazofungwa kwenye kitanzi hutokeza kwenye uke kupitia mlango wa mji wa mimba. Mtumiaji anaweza kugusa nyuzi hizo kama anataka kujua kama kitanzi alichoweka bado kipo. 2. Zipo aina mbili tu za Vitanzi
a) LNG – 20 (Levonorgestrel) huitwa pia mirena, husambaza – dawa ya LNG ambayo ni aina ya projestrone.
Kitanzi hiki kina uwezo mkubwa zaidi kuzuia mimba kuliko cha shaba, na kufanya kazi kwa miaka 5.
b) Kitanzi cha Shaba (Copper IUD ) :- Copper T 380- A
Kinatumika sana katika soko .
Waya wenye madini ya shaba, kuzungushiwa kwenye shina la kitanzi lenye umbo la T.
Inafanya kazi kwa miaka 10, na ina nguvu sana.
3. Utendaji wake
Aina zote za Vitanzi huzuia mimba kutokana na kuharibiwa kwa tumbo la uzazi ambamo mtoto angekaa, hivyo vinaua mimba changa.
Kufanya ute wa mlango wa tumbo la uzazi mgumu, hivyo kuzuia mbegu kupita.
Inazuia ukuaji wa ngozi nyororo ya tumbo la uzazi (Endometrium) na hivyo kuzuia mtoto kujipandikiza
Mtoto akishafika hapo, hawezi kujipandikiza, anakufa, na masalia yake yanatoka pamoja na damu ya mwezi
Kitanzi cha shaba, hutengeneza sumu kwa mbegu kikiwa katika mji wa mimba hutoa sumu ambayo huua mbegu.
4. Utaalamu
Kabla ya kuwekewa, mwanamke anapaswa kupima nyonga, matiti majimaji ya ukeni, magonjwa ya zinaa na kama ni mjamzito.
Vitanzi huwekwa na watu waliosomea fani ya uganga.
5. Uwezo wake
Kutumia LNG, mwanamke 1 kati ya 100, anapata mimba. Katika miaka 5, kwa wanawake mia, wanawake 7 wanapata mimba.
Ukitumia Copper T, wanawake 6 kati ya 1000 wanapata mimba, kwa miaka 10, wanawake 20 mpaka 30 wanapata mimba katika kila wanawake 1,000.
NB : Kwa vile inafahamika kuwa kitanzi kinaharibu ngozi nyororo ya mji wa mimba, sehemu muhimu ya mtoto kutunzwa na kukua, basi uwezo wa kitanzi katika kuua watoto hao ni mkubwa. Hivyo kitanzi huua watoto wengi zaidi katika mwaka. 6. Madhara
Matatizo ya hedhi kutokana na kutoa damu nyingi na michubuko
Kutoka damu matone matone , au damu kidogo sana wakati wa hedhi
Vyaweza kutoboa au kuchana au kuzama katika tumbo la uzazi
Kusukumwa nje ya tumbo la uzazi
Saratani ya matiti / kulainika matiti, mabadiliko ya tabia
Kuumwa kichwa
Kuumwa miguu
Madhara makubwa
Kutopata au kuchelewa kupata hedhi
Kutoka damu nyingi
Maumivu makali wakati wa ngono
Maambukizo ya magonjwa ya zinaa na ukimwi
Kutoa harufu mbaya ukeni
Homa kali hadi zaidi ya 38%
Utoaji wa mimba: ushahidi unaonyesha kuwa mimba nyingi zinatolewa kwa wanawake waliowekwa vitanzi walao mara tatu kwa mwaka.
Vitanzi husababisha kuzaliwa watoto kabla ya umri wao pamoja na kuzaliwa watoto wakiwa walemavu. Baadhi huzaliwa na vitanzi maungoni.
Vitanzi chaweza kujizamisha katika ngozi laini ya tumbo la uzazi.
Husambaza mwilini sumu ya shaba (Copper toxicity).
Maumivu ya miguu au uvimbe wa miguu.
Kukosa hamu ya tendo la ndoa.
7. Wanawake wenye hali zifuatazo wasitumie Vitanzi
Wajazito
Wenye magonjwa ya zinaa
Watokao damu
Wenye kasoro za tumbo la uzazi
Wenye maambukizo ya tumbo la uzazi bila kujua sababu zake.
Ambao mwili wao una matatizo (allegic) na shaba
8. Hatari za baadaye ziletwazo na kitanzi
Ingawa wanawake wengi wanapoacha kutumia vitanzi wanaweza kupata ujauzito baadaye, vitanzi vinaweza kuwa na athari kubwa sana juu yao. Ikiwa ukuta wa tumbo la uzazi utadhurika, utavimba au utachanika, mji wa mimba na mirija ya uzazi vinaweza kuharibika na kuathiri uwezo wa kupata ujauzito. Pale ambapo madhara ya kitanzi yamekuwa makubwa inabidi kuondolewa kizazi, ambapo mwanamke hataweza tena kupata mtoto. Pia chachu bandia zinazokuwepo kwenye kitanzi zinasababisha uchelewaji wa kupata hedhi na uzazi baada ya kuondolewa vitanzi.
TAMKO LA WAFAMASIA WATETEAO UHAI KUHUSU VITANZI
Sio sahihi kukengeusha taarifa za kisayansi ili zitumikie itikadi fulani ambazo zina lengo la kuushambulia uhai wa binadamu.
Tafiti kuhusu utendaji wa Vitanzi unaonyesha kuwa ngozi nyororo ya tumbo la uzazi huharibiwa na uwepo wa vitanzi au kemikali hiyo. Hali hiyo husababisha mtoto ashindwe kujipandikiza, hivyo mtoto huyo anakataliwa na kufa.
Uongo unaoenezwa kuwa vitanzi ni vidhibiti mimba badala ya kuwaeleza watu kuwa vitanzi ni viua–uhai ni kinyume na maadili ya kitaaluma. Ili ‘‘mteja’’ aweze kuchagua kuwekewa kitanzi ni lazima kwanza aelezwe ukweli wote kuhusu kifaa hicho, kufanya kinyume chake ni kuwanyima ‘‘wateja’’ uwezo wa kuamua kwa hiari yao.
Chanzo cha habari
1. The Essentials of Contraceptive Technology (1997)
2. The Facts of Life (1997)
3. Modern Contraception updates from the Contraception Report (1997).
4. Human Life International, 4 Family Life, Font Royal, Virginia 22630