1. Utangulizi
Mashirika yanayoendeleza njia za kisasa za kupanga uzazi zinasifia vipandikizi (norplant) kama ni njia nzuri na salama kwa wanawake wanaotumia. Mashirika hayo yanadai kuwa njia hii ni ya rahisi kwani inaondoa ile adha ya kumeza vidonge kila siku, zoezi ambalo baadhi ya watumiaji husahau. Sifa kubwa ni kuwa ina uwezo mkubwa wa kuwafanya tasa mamilioni ya wanawake katika nchi zinazoendelea.
2. Vipandikizi ni nini?
Hii ni chachu (hormone) iitwayo ‘‘levonorgestrel’’ inayowekwa katika vifuko – 6. Baada ya kuwekwa, chachu hii huanza kufanya kazi masaa 24 hadi miaka 5. Kila kifuko huwekwa mg 36 za chachu ya ‘’crystalline levonorgestrel’’ na kila kifuko kina urefu wa mm 34 na upana wa mm 2.4. Kiasi mcg 30 ya projestini husambazwa katika damu kila siku.
Aina nyingine ya Vipandikizi ni ile iitwayo Norplant II yenye vifuko 2 na Implanon yenye kifuko kimoja.
Vikiwekwa mwilini, vipandikizi hivi hudumu kuanzia miaka 2 hadi 3. Vipandizi hivi hufanya kazi sawa sawa na vidonge vya majira, ila vina uwezo mkubwa wa kuua mimba changa kutokana na kuharibu ngozi nyororo ya mji wa mimba.
3. Utendaji wake
Vikiwa ndani ya mwili vipandikizi hufanya kazi zifuatazo :
kuzuia yai kukomaa na kuchopoka kutoka katika kokwa.
Kuzuia utengenezaji na ukuaji wa ngozi nyororo ya tumbo la uzazi.
kugandisha ute wa mlango wa tumbo la kizazi
Vipandikizi hivi huwekwa kwenye mkono wa mwanamke baada ya kufanyiwa operesheni ndogo katika ngozi yake sehemu ya chini ya kiwiko cha juu cha mkono.
Vipandikizi hutengenezwa na kampuni ya WYETH AYERST ya Marekani chini ya usimamizi wa Halmashauri ya idadi ya watu na kugharamiwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID)
Madhara ya vipandikizi ya kawaida
a) Madhara ya kawaida
Mabadiliko katika hedhi
Kutoka damu kidogo sana na hakuna damu kabisa
Kuongezeka uzito kati ya 2 na 5 kwa mwaka
Kunyonyoka nywele katika paji la uso.
maumivu ya miguu
mabadiliko ya tabia (huzuni au wasiwasi mkubwa)
b) Madhara makubwa yanayohitaji matibabu ya haraka
Kutoka damu nyingi
Kutoka damu ya mwezi kwa muda mrefu
Kutotoka damu kabisa
Maumivu makali kwenye kinena
Kuumwa kipanda uso au maumivu makali ya kichwa
kuadhirika sehemu iliyowekwa vipandikizi (Kuwa pekundu , kuvimba au kutoka damu)
c) Wanawake wengine waliotumia vipandikizi walieleza matatizo yafuatayo
Matatizo ya kuona mianga mianga, kuona kidogo au kutoona kabisa.
Mabaka mabaka mwilini
Kukosa hamu ya tendo la ndoa
Matatizo ya moyo
Kichefuchefu
Mkandamizo wa damu
Uchovu
Kupungua uzito
Kizunguzungu
Mtaalamu Farida Akhter na mwengine ameongeza kuwa watumiaji wa vipandikizi kupoteza fahamu mara kwa mara
5. Wanawake wenye hali zifuatazo za kiafya wasitumie vipandikizi ?
Wenye kuhisi kuwa ni waja wazito.
Watokao damu ukeni bila kufahamu sababu zake
Wenye magonjwa ya maini
Wenye dalili ya saratani ya matiti
Wenye matatizo ya miguu
Chanzo cha habari Population Research Institute, Review May/June 1996
Brian Clowes, PhD The Facts of Life, (2nd Ed.), 2001 Human Life International
The Essentials of Contraceptives Technology, A Handbook for Clinic Staff, Johns Hopkins Population Information, 1997 Health, Psychological and Moral hazards caused by hormonal contraceptives