1. MAANA
Vidonge vya majira ni aina ya vidhibiti mimba vitumiavyo chachu za bandia za projestorini na estrojeni zilizotengenezwa katika maabara ambazo hutumia vidonge ambavyo mwanamke humeza kila siku. Zipo aina mbalimbali za vidonge. Majina ya vidonge hutegemea aina na kiwango cha chachu zilizowekwa. Vidonge vyenye chachu ya estrojeni pekee huitwa tu « vidonge », kwa kiingereza « The Pill ». Vidonge vyenye mchanganyiko wa chachu ya estrojeni na projestini huitwa « vidonge mchanganyiko, « Combined Oral Contraceptives » [COC]. Vidonge vyenye aina chachu ya projestini pekee huitwa « Progestorene Only Pills [POP] au «Low Dose Pill » au « Mini Pill ». Leo hii vidhibiti mimba vingi vimetengenezwa kwa chachu hii pekee [kama vile « Morning After Pills », RU486, Emmergency Contraceptives].
2. CHACHU ZA ASILI
Mungu amempa mwanamke chachu mbili za uzazi, nazo ni estrojeni na projestorini ambazo hutenda kazi yake kwa kusaidiana na kutegemeana. Chachu ya estrojeni, ambayo kwa asili huhusika na uundwaji wa silika ya kike na kuidumisha, hutengenezwa wakati wa kuiva kijiyai. Chachu hii inachukuliwa na damu katika ngozi nyororo ya tumo la uzazi na kuiamsha kukua na kujitayarisha kupokea mtoto. Pia estrojeni inachukuliwa kwenye mlango wa tumbo la uzazi kuamsha vikunjo kutengeneza ute wa uzazi. Baada ya muda kijiyai kinachopoka na kupokelewa na mirija. Iwapo yai hilo litakutana na mbegu ya kiume, basi mimba hutokea ; kama halijakutana na mbegu ya kiume, huharibika baada ya masaa 24 na kuyeyuka palepale kwenye mirija. Kijifuko cha kijiyai kinabaki, huitwa sasa Corpus Luteum na kutengeneza chachu za estrojeni na projestini.
Chachu ya projestorini inaamsha ngozi nyororo ya tumbo la uzazi kujitayarisha kumpokea mtoto aliyetungwa katika mirija ya uzazi. Pia inachochea vikunjo vya chini vya mlango wa tumbo la uzazi kutengeneza ute mzito sana, ili kufunga mlango wa tumbo la uzazi mpaka hedhi inapoanza au mpaka kuzaa, mama anapopata mimba. Tena inaamsha vishimo vidogo vidogo [pockets of shaw] ukeni kukausha ute wa uzazi.
4. UTENDAJI WA ESTROJENI NA PROJESTINI
Chachu za estojeni na projestini bandia zinazotengenezwa katika maabara hufanya kazi zifuatazo azitumiapo mwanamke.
Chachu bandia ya estrojeni huzuia yai kukomaa na hivyo kuzuia uwezekano wa kutunga mimba.
Chachu bandia ya projestoreni hudumaza ukuaji wa ngozi nyororo au pia huharibu ngozi nyororo na hivyo hushindwa kupokea mimba na mtoto hufa kwa kukosa lishe na hewa na kutoka na damu ya mwezi wiki mbili baadaye.
Chachu bandia za estrojeni na projestini hufanya ute kwenye mlango wa kizazi kuwa mzito na hivyo mbegu hushindwa kupita.
Kwa hiyo vidonge vyenye chachu mchanganyiko wa estrojeni na projestini hufanya kazi mbili kwa wakati mmoja - kuzuia mimba na kuua binadamu mpya.
5. VIDONGE VINA UHAKIKA?
Kinadharia vidonge hufanya kazi kati ya 95% - 99%. Hii ina maana kati ya wanawake 100 wanaotumia vidonge, 1-5 wanapata mimba katika mwaka mmoja. Lakini uzoefu unaonyesha kuwa kati ya wanawake wanaotumia vidonge 1.9% - 18.1% hupata mimba bila ya wao kutegemea.
6. VIDONGE NI SALAMA?
HAPANA NDUGU Vidonge na dawa zote zitumikazo kwa kupanga uzazi zina madhara makubwa kwa watumiaji.
1. Madhara katika damu na moyo
Kuganda damu damu inaweza kuganda na hivyo kuzuia damu kutembea na hivyo kuhatarisha maisha. Mathalani, iwapo damu imeganda katika moyo inaweza kusababisha ugonjwa wa moyo, katika ubongo itasababisha kupooza (Stroke) au ubongo kutoka damu, damu iliyoganda sehemu nyingine ya mwili inaweza kuharibu mapafu, figo, katika mishipa ya macho inasababisha upofu. 2. Mkandamizo wa damu
Hasa kwa wanawake wanaovuta sigara na wale wenye umri unaozidi miaka 35. 3. Saratani
Wasichana wanaotumia vidonge vya majira kabla ya kufikia umri wa miaka 25, asilimia 25 yao hupata saratani ya matiti. Baadhi ya dalili za saratani ni matiti kuwa laini, makubwa, vivimbe na kutoka maziwa mfululizo.
Saratani ya njia ya kizazi hutegemea muda wa matumizi na kiwango cha kujamiiana, kama anavuta au la, usafi na idadi ya wanaume aliojamiiana nao. Matumizi ya vidonge yameongeza kiwango cha uasherati na uwezekano mkubwa wa kupata magonjwa ya zinaa, ukiwemo UKIMWI.
Saratani ya tumbo la uzazi na kokwa ambayo hutokea hasa kwa wanawake waliotumia vidonge mchanganyiko na hasa kwa wanawake waliopita muda wa kuzaa.
Saratani ya ngozi, kama vile mabaka mabaka
4. Uvimbe katika figo
Hutokea hasa miongoni mwa wanawake wa umri wa miaka ya kati ya 15 na 35 hasa kwa wanawake waliotumia zaidi ya miaka minne.
5. Hedhi isiyo ya kawaida
Baadhi ya wanawake wanaotumia vidonge wanapata hedhi isiyo na mpangilio au kutopata hedhi kabisa. Wengine wanapata maumivu makali wakati wa hedhi.
7. Kupima
Kabla ya kutumia vidonge vya majira, yafaa sana wanawake wapime kwanza afya zao na kuchukua tahadhari kubwa. Wanawake wenye matatizo yafuatayo wasitumie:
Wenye magonjwa ya moyo
Wenye shinikizo la damu
Wenye historia ya kuganda damu
Wenye magonjwa ya zinaa
Wenye kuumwa kichwa mara kwa mara
Wenye matatizo ya kuona
Wenye ngozi au macho ya njano wakati wa ujauzito
Wanawake wenye umri mdogo wasitumie kabisa kwa sababu ya hatari ya madhara wakati wa umri mkubwa.
Chanzo cha habari
1. The Coupe to Couple League Inc.
P.O. Box 111184, Cincinnati
OH45211-1184 USA
2. Dr. Robin Bernhoft, Contraception; Empty Promises ‘Trail of Tears’, Global Family News
August 2002/Vol 1, No 4
3. Uimarishaji wa Familia, Mpango wa Uzazi kwa njia ya asili, Billings Ovulation Method,
Toleo la 5, 2005
Sista Birgitta Schnell OSB, M.D. Surgeon