UWINGI WA WATU KICHOCHEO CHA MAENDELEO
Na Emil Hagamu
Kufikia Septemba 2013 Afrika, ambayo ndiyo bara duni kuliko yote duniani itakuwa na kiwango kikubwa cha ukuaji wa idadi ya watu kuliko bara lingine lolote kati ya sasa na 2050
Inakadiriwa kuwa kasi ya ukuaji wa idadi ya watu itakuwa mara dufu, ikiongezeka kutoka bilioni 1.1 ya sasa hadi bilioni 2.4 ifikapo 2050. Kwa kiasi kikubwa ukuaji huo utatokea katika nchi 51 zilizo maskini zaidi za Afrika zilizo katika ukanda wa Sahara. Taarifa ya Wendy Baldwin, rais na mtendaji mkuu wa shirika hilo zinaendelea kusema kuwa, ukuaji huu wa idadi ya watu unazuia uwezo wa uchumi kutengeneza ajira na kuinua hali ya maisha ya watu kutoka umaskini wao.
Leo, wanawake katika ukanda wa Sahara wa Afrika wana uzao wa wastani wa watoto 5.2, kiwango kinachopanda hadi kufikia 7.6 katika nchi ya Niger. Nchi 10 zenye viwango vya juu vya uzazi ziko katika ukanda wa Sahara wa Afrika. Zaidi ya kuwa na viwango vya juu vya vizazi, idadi kubwa ya watu katika sehemu hiyo bado vijana, ambapo asilimia 43 ya watu wako chini ya miaka 15.
“Kwa kuzingatia kuwa idadi kubwa ya watu wake ni vijana, ukuaji wa idadi ya watu katika utategemea viwango vya matumizi ya vidhibiti mimba kwa wazazi wa baadaye”, anasema Carl Haub, mkuu wa kitengo cha idadi ya watu katika shirika hilo la Population Reference Bureau. Anaendelea kusema kuwa viwango vilivyotajwa vya ukuaji wa idadi ya watu utategemea jinsi matumizi ya vidhibiti mimba yatakavyokuwa yamekubalika zaidi. Kama si hivyo, basi idadi ya watu Afrika itaongezeka kwa kasi zaidi, ikitishia jitihada za kuondoa umaskini, kutengeneza ajira na kutunza mazingira.
Takwimu za idadi ya watu zinaeleza kwa kina taarifa kuhusu afya na mazingira katika nchi zaidi ya 200 zikionyesha zaidi tofauti za utajiri na kipato. Nchi zinazoendelea zinaonyesha pengo kubwa kati ya matajiri na maskini zikihusishwa na tofauti za kizazi na afya. Kwa mfano, nchini Uganda, wanawake 1/5 ya familia za watu maskini wana watoto mara mbili zaidi ya wale wa 1/5 ya familia za watu matajiri. Na watoto wengi kutoka familia za watu maskini wanakufa kabla ya miaka 5 kuliko wenzao wazaliwao katika familia za watu tajiri.
Nchi za Niger na Netherlands [Uholanzi] zimechukuliwa kama mfano wa tofauti kubwa kati ya nchi maskini na tajiri. Ingawa nchi hizo zina idadi ya watu sawa, inakadiriwa kuwa idadi ya watu wa Niger itakua mara tatu zaidi kutoka milioni 17 ya leo hadi milioni 66 kufikia 2050. Wakati idadi ya watu Netherlands itakua kutoka 17 ya leo kufikia milioni 18 ifikapo 2050. Viwango hivyo vitatokana na tofauti ya wastani wa uzao kwa kila mwanamke na ulinganifu wa uzao katika umri wa uzazi. Kiwango cha uzao wa watoto 7.6 ni mara tatu zaidi ya kile cha Netherlands cha uzao wa watoto 1.7 kwa kila mwanamke. Nusu ya idadi ya Niger ni vijana chini ya umri wa miaka 15, wakati asilimia 17 ya idadi ya watu wa Netherlands.
MASUALA MENGINE MUHIMU KUHUSU IDADI YA WATU 2013
UKUAJI WA IDADI YA WATU KIMABARA
Afrika
Kufikia 2050 idadi ya watu inakadiriwa kufikia 2.4 bilioni kutoka 1.1 ya sasa, na kulifanya bara hili kuwa lenye kiasi kikubwa cha ukuaji wa idadi ya watu kuliko mengineyo yote. Hata hivyo viwango hivi vitategemea ukweli kuwa ukuaji wa wake utapungua taratibu katika nchi zote za Afrika kama ambavyo vizazi viliporomoka katika mabara mengine. Na mategemeo hayo yatajikita katika ukweli kuwa matumizi ya vidhibiti mimba yatakubalika na kutumiwa zaidi barani Afrika. Kwa hali ya sasa viwango vya kizazi havitashuka sana katika nchi nyingi na pengine havijashuka kabisa. Na hata kama viwango vya kizazi vitapungua, bado idadi ya watu itaongezeka baada ya 2050 kwani wengi watu wake watakuwa vijana.
Asia
Bara hili ni makazi kwa asilimia 60 ya watu wote duniani. China na India hubeba nusu ya idadi ya watu barani Asia. Viwango vya kizazi nchini China ni vya chini sana 1.5 kwa kila mwanamke. Kama China itashituka kwa kubaini ukweli kuwa idadi kubwa ya watu wake ni wazee na kulegeza masharti yake ya uzao wa mtoto mmoja, basi makadirio ya idadi ya watu yatakwenda juu. Nchini India viwango vya kizazi vimeporoka kutoka 5.5 kufikia 2.4 kwa kila mwanamke. Majimbo ya kaskazini mwa India bado yana viwango vya juu vya kizazi, ingawa majimbo hayo bado ni maskini sana. Pamoja na hayo, inakadiriwa kuwa India itaipiku China katika wingi wa watu katika miaka 15 ijayo na kuwa nchi yenye watu wengi zaidi duniani, bilioni 1.5.
Amerika Kusini/Caribbean
Ukuaji wa idadi ya watu umekuwa ukishuka taratibu katika bara hili, kwa kiasi kikubwa kutokana na kupungua kwa vizazi, hasa Brazil na Mexico, nchi mbili zenye jumla ya idadi ya watu zaidi ya nusu ya watu wote wa eneo hili. Viwango vya vizazi kwa Brazil ni watoto 1.8, wakati kule Mexico ni 2.2. Miongoni mwa nchi zinazoendelea Amerika ya Kusini/Caribbean ndizo zenye kuwa na viwango vya juu vya utumiaji wa uzazi wa mpango, kwa asilimia 75 kwa njia zote na asilimia 68 kwa vidhibiti mimba kwa wanawake walioolewa. Idadi ya watu katika eneo hili inakadiriwa kuongezeka kutoka milioni 606 ya sasa hadi milioni 780 ifikapo 2050. Watu wakaribiao robo tatu milioni huhama nchi hizi kwenda kuishi Marekani na Ulaya kila mwaka.
Amerika ya Kaskazini
Amerika ya Kaskazini na Canada kwa pamoja wana viwango vya chini vya kizazi; Canada 1.6 na Marekani 1.9. Katika kipindi cha kudorora uchumi siku za karibuni, viwango vya kizazi viliporomoka zaidi hasa miongoni mwa Wahispania. Wahamiaji wanaleta faida katika ukuaji wa idadi ya watu katika nchi zote, Marekani na Canada.
Ulaya
Imeshuhudia kuporomoka kwa kasi kwa viwango vya kizazi katika miongo ya hivi karibuni. Inakadiriwa kuwa kutakuwa na kupungua kwa idadi ya watu barani humo kutoka milioni 740 ya sasa na kuwa milioni 720 ifikapo 2050, na hata idadi hiyo ndogo itategemea wahamiaji ambao wanatarajiwa kupunguza kasi ya uporomokaji wa kasi wa idadi hiyo ya watu. Siku hizi wanawake wa Ulaya wanazaa wastani wa watoto 1.6, ukilinganisha na watoto 2.6 miaka ya 1960. Vizazi hivi vya chini vimesababisha kuwa na idadi kubwa ya watu kuzeeka. Huko Ulaya idadi ya watoto walio chini ya miaka 15 ni asilimia 16 tu. Ukilinganisha hali hiyo na Afrika, utaona kuwa idadi ya watoto walio chini ya miaka 15 ni asilimia 41 na asilimia 25 kwa bara la Asia. Viwango vya wazee wenye miaka 65 na zaidi vitapanda kwa zaidi ya asilimia 27 kufikia 2050
Oceania
Huko Australia na New Zealand, inategemewa kuwa idadi ya watu itaongezeka kutokana na wahamiaji. Viwango vya kizazi kwa Australia ni 1.9; New Zealand 2.0. Huko Australia, idadi ya watu inategemea kuongezeka kufikia milioni 34 ifikapo 2050 kutoka idadi ya sasa ya milioni 23. Wakati huo huo idadi ya watu huko New Zealand itaongezeka kufikia karibu milioni 6 ifikapo 2050 kutoka idadi ya sasa ya milioni 4.5
(Taarifa hii inatoka Shirika la Idadi ya Watu (Population Reference Bureau) la Marekani)
TAFSIRI YA TAARIFA HII
Ndiyo maana kwa muda mrefu sasa nchi hizo zimekuwa na mikakati ya kuchochea wanawake kuzaa watoto wengi ili kufidia upungufu unaoendelea kujitokeza. Mikakati hiyo ni pamoja na kumlipa kila mama mzazi posho ya uzazi na kutoa malipo kwa kila mtoto anayezaliwa baada ya watoto wawili kama motisha ya kuendelea kuzaa zaidi,likizo ya uzazi ya miaka 3, likizo ya uzazi kwa akina baba yenye malipo pia, kuzipatia familia zenye watoto wengi upendeleo wa mafao ya kibima [kama vile bima ya afya] na kukaribisha wahamiaji kutoka mataifa mengine. Nchini Urusi ambako idadi ya watu imeporoka kwa kiasi kikubwa sana, serikali imeanzisha programu za njia za maumbile katika mpishano wa uzao badala ya kutumia vidhibiti mimba. Vilevile nchi hiyo imefutilia mbali sheria ya kutoa mimba na kupiga marufuku ushoga [ni kosa la jiai kutoa matangazo kuhusu ushoga, au mtu kusimama hadharani na kutetea ushoga]. Serikali ya Urusi imetoa wito kwa wanandoa kuzaa watoto wengi.
Katika nchi nyingine serikali zimeanza kutoa upendeleo kwa akina mama kutofanya kazi ili wabaki nyumbani kwa malezi ya watoto. Familia zinazoamua kufanya hivyo hulipwa fidia kwa mama kutofanya kazi. Wito umetolewa kwa wazazi kufahamu elimu ambayo watoto wao wanafundishwa shuleni na kuwa na uhuru wa kumwondoa mtoto shuleni kama elimu anayopata haiendani na maadili ya familia. Kwa hiyo masomo ya ngono yameamanza kupigwa vita na programu za elimu ya maadili zinaanza kuingizwa tena katika mitaala ya elimu
KWA NINI NCHI ZA AFRIKA HAZIPIGI HATUA KUBWA KIMAENDELEO?
HOJA ZA UWONGO
Kwa miaka yote watu wa nchi zinazoendelea, wakiwamo Watanzania, wameaminishwa, nao wakaamini, kwamba umaskini wetu unatokana na kuzaliana kwetu, yaani idadi kubwa ya watu wanoongezeka kila mwaka. Ni kwa msingi huo baadhi ya viongozi wa Kiafrika, wamesikika wakiwashauri wananchi wao kupunguza kuzaliana. Katika sensa ya mwaka jana [2012] tuliambiwa kuwa sasa idadi yetu imefikia milioni 45 kutoka milioni 35 miaka kumi iliyopita, na wanasiasa wakatumia sensa hiyo kututisha kwamba idadi hiyo ni kubwa mno kwa maendeleo ya nchi yetu, na kwamba kuendelea kuzaliana zaidi kutazidi kutuongezea umaskini. Hata tukasikia wito wa kuongeza viwango vya matumizi ya vidhibiti mimba kutoka asilimia 24.7 hadi asilimia 60 ifikapo 2015. Nilikanusha hoja hizo katika nafasi mbalimbali, na kuanzia leo nitakuwa natoa ushahidi kwamba umaskini wetu hautokani na kuongezeka kwetu, bali unatokana na sababu zilizo nje na hata ndani ya mamlaka yetu.
KWA NINI VIZAZI NA IDADI YA WATU KATIKA NCHI ZILIZOENDELEA INAPUNGUA
UKWELI WANAOFICHA
Kabla hatujaendelea kujadili hoja hiyo, kwanza tujiulize kuporomoka kwa vizazi na idadi ya watu katika nchi za Magharibi na nyingine za Mashariki kumetokana na nini? Hakuna Mmarekani, wala Mzungu, wala mtu wa Asia atakayekuambia kuwa kuporomoka kwa vizazi kumetokana na sababu kuu sita zifuatazo: matumizi ya vidhibiti mimba, utoaji mimba, kufunga kizazi, elimu ya ngono, ushoga na umame. Badala yake wao wataendelea kutuaminisha kuwa viashiria vya maendeleo ni kuwa na idadi ndogo ya watu ambao wanatokana na familia ndogo ya watoto mmoja au wawili. Haya yakitimizwa basi watu watajenga nyumba nzuri, watanunua magari ya kutembelea, watoto watapata elimu bora, familia zitakuwa na uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Ukweli ndio huu:
Ingawaje matumizi ya vidhibiti mimba, kama vile kondomu, yametumika miaka mingi kabla ya uvumbuzi wa vidonge vya majira na njia nyingine, nguvu kubwa ya matumizi ya vidhibiti mimba iliwekwa na mwasisi wake, Margaret Sanger wa Marekani ambaye anajulikana kama ‘Baba wa Kizazi Kipya’ na Marie Stopes wa Uingereza ambaye ni mashuhuri kwa utoaji mimba ambaye ameyageuza matumbo ya wanawake kuwa machinjio. Kwa kadiri yao, lengo la vidhibiti mimba halikuwa KUPANDA UZAZI kama watu wanavyodanganywa, bali, lengo lake lilikuwa KUDHIBITI KIZAZI, yaani kuharibu ile sehemu muhimu ambapo kila binadamu hupitia ili, yaani kizazi cha mwanamke kwa lengo la kukomesha kuzaliana. Matumizi ya vidhibiti mimba yalipata umaarufu kutokana na nadharia za ukombozi wa wanawake zilizoanza huko Marekani, Kanada na Uingereza mwanzoni mwa karne ya ishirini.
Matumizi ya vidhibiti mimba yalipata umaarufu baada ya kuvumbuliwa vidonge vya majira mnamo miaka ya 1960 na kuchochewa na uwongo wa Paul Ehrlich katika kitabu chake “The Population Bomb” cha 1968. Katika kitabu hicho Paul Ehrlich aliandika kuwa idadi ya watu ilikuwa inaongezeka kama mlipuko wa bomu na hivyo alihofia dunia kujaa na bila kufanya jitihada za kudhibiti kasi hiyo ya ongezeko la idadi ya watu basi idadi kubwa ya watu ingesababisha uharibifu wa mazingira, njaa, joto na vita. Kuanzia miaka hiyo matumizi ya vidhibiti mimba yamechukuliwa kama ishara ya ustaarabu na maendeleo na ukombozi wa wanawake. Kwa kadiri wanawake walivyokinai kuzaa ndivyo hivyo walijiona huru zaidi kutokana na vifungo vya ndoa, uzazi, kunyonyesha na kulea. Pia kwa vile wanawake walikuwa wazazi waliowajibika kuwalea watoto wakiwa nyumbani, vidhibiti mimba viliwafungulia milango ya kufanya kazi za ajira, ambazo ziliwazuia kuzaa au kuzaa watoto wachache na kwa mpishano wa muda mrefu ili kutoa nafasi kubwa kwa kazi na kipato. Na hapo ndipo idadi ya watu ilipoanza kupungua, kwani kadiri walivyozaa watoto wachache ndivyo idadi yao katika familia na taifa ilivyopungua. Zaidi ya hayo vidhibiti mimba viliwajengea wanawake chuki dhidi ya uzazi na uzao, wakipendelea zaidi tendo la ndoa kwa ajili ya kujifurahisha kuliko kuzaa mtoto. Wakati mwingine matumizi ya vidhibiti mimba yamehusishwa na mmomonyoko wa maadili [vitendo vya uasherati] na wanawake kupatikana kama bidhaa sokoni na hivyo kutumiwa na wanaume kama vyombo vya starehe.
Mtu mmoja alipata kusema miaka kadhaa ya nyuma kuwa ‘bila kuweka sheria za kutoa mimba katika nchi idadi ya watu haiwezi kupungua’. Alimaanisha kuwa ili idadi ya watu ipungue, ni lazima mataifa yakubali kutunga sheria za kutoa mimba. Utoaji mimba huua maelfu na hata mamilioni ya watoto ambao bado hawajazaliwa. Kwa lugha ya sasa, kama ingekuwa wanaouawa ni watu wakubwa, basi ingestahili kuitwa mauaji ya halaiki. Na wale wanaotengeneza vifaa vya kutolea mimba wangejulikana kama watengenezaji wa silaha za maangamizi ya halaiki. [Sadam Hussein na viongozi wengine katika nchi mbalimbali walishambuliwa na kuuawa kwa kuwa walisadikiwa kuua watu kwa maelfu na kutengeneza silaha za maangamizi] Maana yake ni kuwa utoaji mimba huondoa kizazi cha baadaye cha taifa lolote lile. Na utagundua kuwa katika nchi zile zenye sheria za kutoa mimba, vilevile kuna shinikizo la kutumia vidhibiti mimba. Hii ina maana kuwa jitihada zinafanyika kwa wakati mmoja, KUZUIA MIMBA KUTUNGWA na KUUA MIMBA ILIYOKWISHA TUNGWA. Mauaji hayo yanafanyika kwa namna mbalimbali; kwa njia za kienyeji, kwa kemikali na kwa upasuaji au njia nyinginezo. Ukiweka mikakati hiyo pamoja ndipo unashuhudia kuporomoka kwa vizazi kusikoweza kuepukika. Watu wa nchi za Magharibi na wale wa Mashariki walikumbatia sera hizo kwa muda mrefu na sasa wanalalamika kuwa idadi ya watu wao inaelekea kwisha.
Kufunga kizazi kwa wanaume hujulikana kama ‘vasectomy’ na kwa wanawake huitwa ‘tubal ligation’. Hii ni hatua ya juu inayochukuliwa kwa lengo la kukomesha kabisa kizazi. Kufunga kizazi ni njia ya kiharamia ya kuwafanya watu kutozaana. Kinachofanyika ni kukata mirija ya uzazi ama ya wanawaume au ya wanawake ili kuzuia mbegu au yai kusafiri kuelekea sehemu ambapo kama mbegu na yai vingekutana ingetokea mimba, yaani mtoto. Njia hii imetumika zaidi kwa mabavu pale ambapo watu wamekuwa wagumu kutumia vidhibiti mimba au kutoa mimba kama njia za kudhibiti kizazi. Lakini pia njia hii hutumika sambamba na vidhibiti mimba na utoaji mimba ili kuharakisha kupunguza kuzaliana na idadi ya watu. Mara nyingi njia hii inatumika katika maeneo ambayo ama watu wake bado wana imani kubwa kwa Mungu Muumba ama sheria za nchi zao zinazuia kabisa kutungwa sheria za kutoa mimba. Programu za mabavu, zinazoambatana na motisha kwa wahudumu, hutumika katika kuwalazimishwa watu kukubali kufunga kizazi. Wakati mwingine wanaume au wanawake waliofungwa kizazi wanatumiwa kama chambo au vivutio katika kampeni za kuwafanya wengine wakubali kufunga kizazi. Hawa wanaotumika katika kampeni husifia kuhasiwa na hulipwa fedha nyingi na mashirika yanayohamasisha ufungaji kizazi. Mahali pengine viongozi wa serikali na wa vijiji wanapokea malipo makubwa [hongo] ili kuwalazimisha watu wa maeneo yao wakubali kufungwa kizazi. Kizazi kikifungwa, basi uzao nao pia unafungwa na kisha tunashuhudia kukosa uzao na kupungua kwa vizazi na idadi ya watu katika nchi hupungua.
Elimu ya ngono inayofundishwa mashuleni inapandikiza mbegu za uasi dhidi ya uzazi na uzao na inahimiza mauaji ya watoto wachanga kabla ya hawajazaliwa. Katika elimu ya ngono watoto wanafundishwa viungo vya uzazi na jinsi vinavyofanya kazi. Wanafundisha ‘vitendo vya wakubwa’ na jinsi mimba inavyotungwa. Masomo hayo yanaamsha hisia za kingono miongoni mwa wanafunzi na kuwajengea udadisi wa kutaka kujaribu. Baada ya kuamsha hisia na vionjo vyao vya ngono, walimu wa somo la ngono wanawapatia wanafunzi zana za kufanyia ngono bila hofu; wanawaeleza wanafunzi hao kuwa wapo maadui wawili katika elimu yao: mimba na magonjwa ya zinaa. Ili kuepuka mimba na magonjwa ya zinaa lazima watumie vidhibiti mimba. Kwa hiyo tangu utotoni wanafundishwa kuwa mimba ni kitu cha hatari kinachotakiwa kuepukwa kwa gharama zote. Kwa vile vidhibiti mimba vina viwango vya kushindwa, basi pale msichana anapopata mimba anashauriwa kwenda kutoa ili aendelee na masomo. Mhudumu mmoja aliwarubuni wanafunzi wa sekondari fulani hapa Dar es Salaam kwa swali hili: “Nani kati yenu yuko tayari kuwaaibisha wazazi wake kwa kukosa masomo kutokana na mimba?” Kila msichana alijibu kwa sauti kubwa, “Hakuna!!!” Basi yule ‘mhujumu’ [aliyetoka shirika fulani la nje lisilo la kiserikali] akawaambia basi chagueni moja ya njia zilizopo - vidonge vya majira, sindano za depo provera, vipandikizi, vitanzi au kondomu. Wanafunzi walichagua walichokitaka na baada ya kutumia, licha ya kupata madhara, walifeli pia masomo, na wengine wamekosa uwezo wa kuzaa hata leo. Mbaya zaidi ‘mhujumu’ yule aliwatengenezea wasichana hawa mazingira mazuri ya kuwa waasherati na kuwaweka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi.
Wakiongea kuhusu madhara ya elimu ya ngono mashuleni wataalamu kadhaa wamepata kusema:
Ushoga siyo kitu kigeni kwa baadhi ya jamii ya watu hapa duniani. Kilicho kigeni ni ushoga uliorasimishwa, yaani ule unaotungiwa sheria za kuwatambua, kuwalinda mashoga. Ushoga unaodai kuzuia kunyanyapaliwa, na kudai haki ya mashoga kuishi pamoja kama wanandoa. Katika nchi mbalimbali mashoga wamejipambanua kama kundi dogo la pekee linalobaguliwa na hivyo kudai kutungwa sheria kuwalinda. Sote tunaelewa kuwa hakuna uzao unaotokana na mwunganiko wa mashoga. Mwanaume akimwoa mwanaume mwenzake, au mwanamke akimwoa mwanamke mwenzake; au kama nchi zinahimiza vitendo vya ngono baina ya watu wa jinsi moja, ni wazi, hapatakuwa na uzao. Kwa kadiri makundi ya mashoga yanavyoimarika katika nchi, ndivyo hivyo nchi inapungukiwa na uzao wa watoto. Rais wa nchi moja hapa Afrika alishinikizwa kuukubali ushoga kama sharti la kupatiwa misaada ya kimaendeleo. Aliwajibu hivi waliomshinikiza: “Sizuii ushoga wala mashoga, unaweza kuwepo, wanaweza kuoana, lakini nataka nione mimba baada ya miezi 6. Kama sitaziona mimba basi sitaki kusikia habari za ushoga wala mashoga. Ni ujinga na upumbavu”. Washinikizaji walikasirika sana kwa jibu hilo. Lakini ndilo jibu sahihi. Ni upuuzi kuendekeza nadharia kengeushi na potofu za ushoga wakati tunaelewa fika kuwa zinadidimiza uzao.
Huko nyuma nilipata kusema kuwa, umame ni nadharia na vitendo vinavyokinzana na umama. Misukumo ya umame inakataa ndoa, kuzaa na kulea. Inapendelea kufanya kazi za ajira, uhuru wa kingono na kutaka usawa na wanaume katika mambo yote - ajira, michezo, siasa, starehe na hata katika dini na imani. Kama kuna haja ya ndoa, basi umame unapigania haki ya kuwa na ndoa za mikataba, ambapo wanandoa wanakubaliana kuishi pamoja kwa muda fulani, kisha kila mmoja kuamua kuishi apendavyo. Mwiko mkubwa, kwa kadiri ya wamame ni mwanamke kuolewa na mwanaume na kubeba mimba. Ndoa ya kudumu ya mume mmoja inachukuliwa kama kifungo au jela, mahali pa mateso. Umame unataka katika maisha ya ndoa pawe na zamu kati ya mume na mke ya kupika, ya kufua nguo, usafi wa nyumba na hata kwenda kliniki na kulea mtoto. Umame unapigania pia likizo ya uzazi kwa wanaume. Wamame wamejiuliza daima, kwa nini ni wanawake tu wabebe mimba? Ndiyo maana katika kujibu swali hilo, mwanaume mmoja shoga huko Marekani alikubali kubeba mimba akaishia kufa yeye na ‘mimba’ yake. Wamame wangefurahi kama Mungu angewaumba bila uzazi, kwani kwao unaonekana kama balaa ambalo wasingependa kulibeba. Ndiyo maana umame unatoa msukumo mkubwa katika matumizi ya vidhibiti mimba na kutoa mimba. Umame unafurahia matumbo ya wanawake kugeuzwa kuwa machinjio ya watoto. Wakiwa wamejiunga katika mashirika ya hiari, hawa ndio wasukumao sheria za kutoa mimba duniani kote. Na kwa kiasi kikubwa umame umedumisha usagaji. Katika hali hiyo ya wanawake kukataa kuzaa, ni dhahiri kuwa uzazi na uzao havitapewa kipa-umbele katika nchi. Na hapa ndipo inaposimama sababu nyingine kubwa ya kuporomoka vizazi katika nchi za Magharibi
KWA NINI WAAFRIKA WANAENDELEA KUWA MASKINI?
Kwanza napenda nitoe tahadhari kuhusu takwimu tulizozitumia ambazo zimetolewa na Shirika linalojishughulisha na masuala ya idadi ya watu duniani, [Population Reference Bureau]. Kihistoria shirika hili lilianzishwa na Guy Irving Burch 1929 na ni moja ya mashirika kongwe ya udhibiti wa idadi ya watu duniani. Burch alikuwa mwanaharakati wa uzao wa kizazi bora [eugenicist]. Aliamini, akafundisha na kuandika kuwa dunia inahitaji kiasi fulani tu cha watu walio bora. Wakati wa Vita Kuu II Burch alitoa mapendekezo yaliyoeleza kuwa matatizo ya dunia yangeondoshwa kwa kuwafunga watu kizazi kwa nguvu - watu hao ni wale wenye ulemavu na wa kizazi duni. Propaganda za shirika hili kuhusu idadi ya watu ndizo zinazotumika katika kusukuma programu za udhibiti wa idadi ya watu. Chukulia mfano mmoja wapo wa propaganda: “Kwa kuzingatia kuwa idadi kubwa ya watu wake ni vijana, ukuaji wa idadi ya watu utategemea viwango vya matumizi ya vidhibiti mimba kwa wazazi wa baadaye”, anasema Carl Haub, mkuu wa kitengo cha idadi ya watu katika shirika hilo la Population Reference Bureau. Anaendelea kusema kuwa viwango vilivyotajwa vya ukuaji wa idadi ya watu utategemea jinsi matumizi ya vidhibiti mimba yatakavyokuwa yamekubalika zaidi. Kama si hivyo, basi idadi ya watu Afrika itaongezeka kwa kasi zaidi, ikitishia jitihada za kuondoa umaskini, kutengeneza ajira na kutunza mazingira
SABABU ZA AFRIKA KUWA MASKINI
Mwanahistoria mashuhuri Walter Rodney katika kitabu chake “How Europe Underdeveloped Africa” 1972, anasema Bara la Afrika lilikuwa na maendeleo makubwa kufikia karne ya 15, kabla ya ujio wa watu wa Magharibi, akitolea mifano ya Misri, Ethiopia, Nubia, Zimbabwe, nchi za Maziwa Makuu, n.k. Ujio wa wafanyabiashara kutoka Mashariki ya Mbali na Mashariki ya Kati ulianza kuliweka Bara la Afrika katika hali ya kunyonywa. Wafanyabiashara hao walikuwa wanachukua kutoka Afrika vito vya thamani, kama vile pembe za ndovu, almasi na mazao mengine muhimu, wakati wao walileta Afrika bidhaa zisizokuwa na thamani na zilizokwisha tengenezwa, kama vile nguo, shanga, viungo, sahani za udongo, n.k. Mali hizo kutoka Afrika ndizo zilianza kujenga uchumi katika nchi zao wakati huo huo uchumi wa Afrika ukianza kudorora.
Uporaji wa mali ya Afrika ulifanywa pia tena kwa vikubwa zaidi na wafanyabiashara wa nchi za Magharibi kabla ya ukoloni. Wakitumia meli zilizotengenezwa imara kwa ajili ya kusafiria masafa marefu baharini, waliweza kutawala usafiri wote wa majini na kufanikiwa kuweka vitega-uchumi katika bara la Afrika na sehemu za Asia. Watu hawa wa nchi za Magharibi walivamia ndani ya bara la Afrika wakapora mali zilizokuwapo, hasa madini, pembe za ndovu na vito vingine vya thamani na kuvitumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi zao. Katika kusafirisha mali hizo muhimu Waafrika walitumikishwa katika kubeba mizigo tena wakitembea umbali mrefu. Katika hali hiyo, wakati uchumi na maendeleo ya nchi za Magharibi ukiimarika na maendeleo kupatikana, watu wa Bara la Afrika waliendelea kurudi nyuma kimaendeleo na hivyo kuzorota kabisa maendeleo yaliyokuwapo.Huu ukawa ndio mwanzo wa umaskini wa Bara la Afrika na watu wake.
Baada ya kustawi biashara, Waarabu, Wazungu na Wamarekani waliamua kupora nguvu-kazi ya Afrika, yaani watu wa Afrika katika biashara ya utumwa. Waafrika vijana, wenye nguvu na afya walichukuliwa kutoka Afrika, wakibebeshwa mizigo mizito kutoka bara hadi pwani na kupakiwa katika meli kama magunia na kusafirishwa kwenda Uarabuni, Ulaya na Marekani. Wakiwa huko watumwa hao walitumikishwa katika kilimo cha mazao mbalimbali kama vile miwa, pamba na hivyo kustawisha viwanda vya Marekani na Ulaya. Kwa bahati mbaya wale watumwa waliopelekwa Uarabuni waliuawa wote au walihasiwa ili wasiweze kuzaliana. Ni katika kipindi hiki tunashuhudia kuanza kujengwa na kupanuliwa kwa miji ya Ulaya kama vile Bristol, Liverpool, Nantes, Bordeaux na Seville.
Kutokana na utajiri walioupata waliendeleza sekta za elimu, nishati, usafiri na usafirishaji, bandari, viwanja vya ndege, afya na mabenki na viwanda. Benki kama vile Barclay’s ilijengwa kutokana na biashara ya utumwa iliyokuwa ikifanywa na David na Alexander mnamo 1756. Kuanzishwa kwa viwanda barani Ulaya ukawa ndio mwanzo wa mapinduzi ya viwanda na kubadilisha kabisa mwenendo wa kiuchumi kati ya Ulaya na Afrika. Afrika ikawa ndilo Bara la kuzalisha mali-ghafi na nguvu kazi, wakati mazao ya viwandani huko Ulaya yalipata soko hapa Afrika. Huu ukawa mwendelezo wa umaskini wa Bara la Afrika. Wakati mabara ya Ulaya na Marekani yaliendelea kutokana na kujengwa na mali na nguvu-kazi zilizoporwa kutoka Afrika, Afrika ikawa inaendelea kupoteza mali na watu wake. Utajiri wa sasa wa Marekani umetokana na biashara ya watumwa iliyokuwa ikiendeshwa na Ulaya ambapo watu wa Ulaya walihamishia Marekani taasisi zao zote za kibepari kwa kutumia nguvu kazi ya watumwa na baada ya kuwaangamiza wenyeji asilia wa Marekani. Maendeleo ya kiuchumi ya Marekani kufikia katikati mwa karne ya 19 yalitegemea sana biashara ya nje, ambapo biashara ya watumwa ilichukua nafasi kubwa. Kwa mfano katika miaka ya 1830 pamba iliyolimwa na watumwa ilileta faida kiasi cha nusu ya mauzo yote ya nje.
Sio tu kwamba ulikuwa ni mfumo wa kinyonyaji, bali lengo lake kuu lilikuwa kuhamisha faida kutoka nchi tawaliwa kwenda nchi tawala [nchi mama]. Kwa mtazamo wa Kiafrika jambo hilo lilimaanisha uhamishaji wa faida iliyopatikana kutokana na nguvu kazi ya Mwafrika na kutoka katika utajiri wa Afrika. Hiyo ilikuwa na maana kuwa wakati nchi tawala zikiendelezwa na utajiri kutoka Afrika, Afrika yenyewe ilikuwa inarudishwa nyuma kimaendeleo. Ili kufanikisha azma yao watawala walitumia makampuni ya kibiashara kunyonya uchumi wa Afrika. Kazi za makampuni haya zilikuwa kuwatumikisha Waafrika katika kilimo na madini, kupanga bei na kuhamisha faida yote na kuipeleka kwao. Mabenki pia yalitumika katika kuhamisha faida ya kifedha na kuipeleka kwao. Serikali ya kikoloni ilikuwa na majukumu matatu katika kuhakikisha kwamba uchumi wa Afrika unaleta faida katika nchi mama:
Waafrika tunaendelea kuwa maskini kwa sababu tumetawaliwa kiakili. Tumeaminishwa kwamba chochote kinachotoka kwa watu wa nchi zilizoendelea ni kizuri. Tumeaminishwa kwamba suluhisho la matatizo yetu kiuchumi yatapatiwa ufumbuzi na mashirika nyonyaji ya Ulaya na Marekani. Mashirika hayo yanapoingia hapa kwetu yanafanya kazi sambamba na serikali zetu na tumeyapa majina mazuri, wawekezaji, au wadau wa maendeleo. Tumeamini katika Umoja wa Mataifa na mashirika yake, kama vile Benki ya Dunia, Shirika la Kimataifa la Fedha, Shirika la Idadi ya Watu Duniani, Shirika la Afya Duniani, na mengineyo mengi pamoja na washirika wake mashirika ya kimataifa, kama vile International Planned Parenthood Federation [IPPF], Population Council, Population Reference Bureau, Marie Stopes International, n.k; kuwa ndiyo yatatoa majibu kwa matatizo yetu. G.S.N Wanene katika kitabu chake, The ABC of Globalization of Africa: from Black to While, 2003 anasema kuwa umaskini wa Afrika unatokana na Waafrika kutawaliwa kiakili. Lengo la ukoloni wa kiakili ni kumfanya aliyetawaliwa kumtegemea mtawala, na hata kumpenda na kuwachukia marafiki zake. Anatoa mfano huu; “Mtu mweusi alinunuliwa na kutumikishwa utumwani – naye analijua hili. Alitawaliwa wakati wa ukoloni; naye analijua hili, na anamjua aliyemtawala. Hata hivyo, Mtu Mweusi bado anawaamini na kuwategemea Watengeneza Sera Weupe katika uwanja wa kiuchumi, katika midani za mawazo… Hata anamtembelea mtawala mkononi akiwa na kapu la kuombea pesa, akivinjari katika miji mikuu ya Mtu Mweupe. Tabia hii inaweza kuelezwa vizuri tu kuwa Mtu Mweusi ametawaliwa kiakili na kwamba hayuko huru”
Waafrika wamekuwa ombaomba siyo kwa sababu wamekuwa maskini. Bali wamekuwa ombaomba kwa sababu wamefundishwa kuwa hivyo. Viongozi wa Kiafrika, baada ya kuwa wamefundishwa vizuri kuwa ombaomba, ni wagumu sana kudadisi sababu ya mafunzo hayo. Wajibu wao mkubwa ni kutetea mchakato wa ukoloni wa kiakili, kwani wanalipwa kwa kuwa hivyo. Ni kutokana na ukweli huu tunaona kuwa viongozi wa Kiafrika wakipokea na kumeza kila kitu kutoka kwa watawala.
Viongozi na wachumi wa Kiafrika wamefundishwa jambo moja baya na mtawala; kwamba, hawawezi kufikiri na hivyo lazima wamtegemee mtawala katika kutatua matatizo ya nchi zao. Hebu tuangalie mifano michache ifuatayo:
Ili kupata ukubalifu, mtawaliwa anaalikwa katika mikutano na makongamano ya kimataifa yaliyoandaliwa na mtawala kwa ajili ya kuangamiza kizazi cha mtawaliwa na kumpatia mbinu za kuangamiza kizazi cha watu wake. Mtawaliwa akishakubali, mtawala anajaza hospitali zote vidhibiti mimba; anajaza maduka yote ya dawa na ya chakula na nguo vidhibiti mimba, anawapatia Wamachinga vidhibiti mimba wauze barabarani, sokoni, ‘vijiweni’. Wakati huohuo anaondoa au anazifanya kuwa adimu dawa za kweli za kutibu magonjwa mbalimbali kutoka katika hospitali na kuwaambia wagonjwa wakanunue kwenye maduka ya madawa.
Mtawaliwa anaona fahari kutusimulia alikokwenda, aliokutana nao na walichoahidi kutupatia kwa faida yetu. Mtawaliwa anapenda zaidi kualika wawekezaji, ambao kwa kweli ni walewale waporaji waliokuwa wakipora mali zetu kabla ya utumwa, wakati wa utumwa na katika kipindi cha ukoloni na sasa katika ukoloni mambo leo. Wanaonyeshwa yalipo madini, ilipo ardhi nzuri ya kulima na hata ilipo gesi. Mtawaliwa anamwambia mtawala chukua kiasi upendacho ila mimi niachie faida kidogo tu, kiasi cha kuniwezesha kuendelea kupumua.
Waafrika wanaendelea kuwa maskini licha ya utajiri mkubwa uliomo katika Bara lao – madini, mazao ya majini, ardhi nzuri ya kilimo, mbuga za wanyama, hali nzuri ya hewa na rasilimali watu vijana, kwa sababu viongozi wengi wamekumbwa na ubinafsi, uroho na uchu wa mali. Viongozi wachache wanagawana sehemu kubwa ya mali ipatikanayo katika nchi kiasi kwamba serikali wanazoziongoza zinakosa fedha za kuwahudumia watu – vituo duni vya afya, huduma duni za tiba, mitaala mibovu ya elimu, matayarisho duni ya walimu na vitendea kazi, miundo-mbinu mibovu ya barabara, kukosekana na kwa uhakika wa nishati ya umeme, na kudodora kwa ufanisi katika utendaji kazi kunakosababishwa na kukatishwa tamaa na uduni wa mishahara. Kiasi kikubwa cha fedha zinazopatikana katika nchi kupitia vyanzo mbalimbali zinatafunwa na wachache wenye dhamana ya utawala. Kinachofuatia ni kuhatarisha uhai wa wananchi ambao wanakosa tiba na mahitaji mengine ya kijamii. Miaka ya nyuma watu waliokuwa wanatumia kwa njia za ubinafsi mali za taifa waliitwa ‘wahujumu uchumi’, siku hizi neno linalojulikana zaidi kwa watu wa aina hiyo ni ‘mafisadi’. Mafisadi wanapora sehemu kubwa ya pato la taifa na kuwaacha wananchi wakiteseka kimaisha na hata wengine kupoteza maisha. Viongozi wengi wa Kiafrika ni wasaliti wa wananchi wao. Wanaingia katika madaraka ya kisiasa au kiserikali na hata katika mashirika/makampuni ya umma kwa lengo la kujinufaisha na sio kuwatumikia wananchi. Fedha za maendeleo [katika ngazi za kitaifa na manispaa] zinaliwa na wale wanaosimamia maendeleo hayo. Tabia za viongozi wengi wa Kiafrika zinachangia kuendeleza umasikini na vifo vya watu maelfu kwa maelfu.
Idadi ya watu nguzo ya maendeleo ya taifa
Kwa miaka mingi sasa, na hasa katika miaka ya hivi karibuni, serikali za nchi za magharibi zimeweka kipaumbele suala la kudhibiti idadi ya watu katika nchi maskini, ikiwemo Tanzania. Tunaona mikutano ikiitishwa kwa ajili ya kujadili jinsi ya kudhibiti kasi ya ukuaji wa idadi ya watu kwa kutumia vidhibiti mimba na utoaji mimba. Katika mkutano uliomalizika hivi karibuni [Oktoba 2013] hapa kwetu Tanzania na kuhudhuriwa na watu na wadau zaidi ya 450 kutoka nchi na sekta mbalimbali duniani ulipitisha maazimio ya kuongeza kasi ya matumizi ya vidhibiti mimba kufikia asilimia 60 ifikapo miaka ya 2020. Mkutano huu ni ufuatiliaji wa utekelezaji wa mkutano uliofanyika London, Juni 2012 ambao ulidhaminiwa na Melinda Gates na Serikali ya Uingereza, ambapo ajenda kuu ilikuwa jinsi ya kuongeza matumizi ya vidhibiti mimba kwa watu milioni 120 wa nchi zinazoendelea kwa lengo la kile kilichosemwa eti kupunguza vifo vya akina mama na watoto. Mkutano huo ulidhamiria kukusanya dola za kimearikani bilioni 4 ambazo zingegawiwa kwa serikali za nchi zinazoendelea kwa ajili ya kutekeleza maazimio yake. Viongozi wa Tanzania walioshiriki mkutano huo walirudi na azimio la kuongeza viwango vya matumizi ya vidhibiti mimba kutoka asilimia 24.7 ya mwaka jana hadi asilimia 60 ifikapo 2015. Kwa kuzingatia kuwa sasa imebaki miaka miwili tu, sijui kama lengo hili litawezekana. Na labda ndiyo maana sasa uratibu wa matumizi ya vidhibiti mimba unafanyika kwa nguvu katika ngazi zote za serikali kwa kushirikiana na mashirika yanayojishughulisha na udhibiti wa ukuaji wa idadi ya watu duniani, bila kujali umri wa mtumiaji na hata kwa kupuuzia au kudanganya kuhusu madhara yatokanayo na matumizi ya vidhibiti mimba.
Hebu tujiulize, kwa nini suala la udhibiti wa idadi ya watu ni muhimu kwa serikali za nchi za magharibi; kwa nini limekwa kama jambo la kwanza kwao na pengine ndilo jambo pekee wanaloliona kuwa muhimu? Yawezekana yakawepo majibu mengi. Makala kutoka mtandao wa www.africa2000.com unaeleza baadhi ya sababu.
Mnamo 1954 kijitabu kilichoitwa ‘The Population Bomb’ kilichokuwa kinaeleza kuwa ilikuwa jambo la lazima kwa Marekani na mataifa mengine huru duniani kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu kilisambazwa miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa huko Marekani. Kijarida hicho kiliendelea kusomeka kuwa rasilimali nyingi zinazohitajika katika kukuza uchumi wan chi zao zinapatikana katika nchi zinazoendelea ambako idadi ya watu inaongezeka kwa kasi sana ambao wanaweza kufanya mapinduzi dhidi ya nchi zilizoendelea.
Jambo linaloelezwa hapa ni kuwa kwa kadiri idadi ya watu inavyoongezeka katika nchi zenye rasilimali nyingi ndivyo hivyo linajitokeza hitaji la watu hao kutumia rasilimali hiyo kwa faida yao. Ukuaji wa idadi ya watu humaanisha upatikanaji mkubwa wa wafanyakazi, na soko na hivyo ukuaji wa idadi ya watu huharakisha ukuaji wa viwanda, na ukuaji huo utamaanisha kwamba nchi hizo zenye rasilimali nyingi zitanufaika kutokana na ukuaji wa uchumi wao. Ukweli huu unaziweka njia panda nchi nyonyaji ambazo zinaona kuwa zitapoteza uwezo wao wa kufaidika na rasilimali zinazopatikana katika nchi zinazoendelea.
Kwa kadiri ya utafiti uliofanyika kama miaka hamsini iliyopita na kuchapishwa kama kitabu mwaka 1961 kilichojulikana kama ‘Population and World Power’ kilichoandikwa na Katherine Organski and A.F.K. Organski, unasema kuwa lengo la kudhibiti idadi ya watu limo katika uroho wa kushika utawala wa dunia. Upo uhusiano kati ya idadi ya watu na nguvu za kitaifa. Watu, waandishi wa kitabu wanasema, ni rasilimali muhimu kwa taifa lolote lile. Uhusiano kati ya idadi kubwa ya watu na nguvu ya taifa unaonekana bayana. Idadi ya watu ndiyo kigezo kikubwa katika kupima uwezo wa taifa kushawishi, kutoa zawadi, kuadhibu na kutumia nguvu. Taifa lenye askari wengi linakuwa na uwezo wa kushambulia na kujilinda, kutishia na kuzima vitisho vya majeshi mengine, na pia kuweza kutoa msaada wa ulinzi kwa wengine.
Lakini pia jambo la kukumbuka ni kuwa ukuaji wa idadi ya watu umekuwa ni jambo la kihistoria, limejidhihirisha katika mataifa mbalimbali na kwa nyakati tofauti. Kitabu kinasema kuwa ukuaji kasi wa idadi ya watu siyo jambo geni.
Nchi za Ulaya ya Magharibi zilipitia vipindi vya ukuaji kasi wa idadi ya watu kwa kadiri nchi hizo zilivyoshuhudia ukuaji wa viwanda vyake na ndiyo ilisababisha hali ya maisha kuboreshwa. Kuboreshwa kwa maisha kulisababisha:
Ndivyo hivyo idadi ya watu ilivyotumika kama kigezo muhimu wakati wa ukoloni. Waandishi wa kitabu wanasema kuwa uwingi wa watu wao uliosababisha mapinduzi ya kibiashara, kilimo na viwanda ndiyo yaliwapa Wazungu nguvu ya kutwaa na kutawala dunia. Bila kuwa na idadi ya watu iliyoongezeka kwa kasi iliyoambatana na ukuaji wa kiuchumi wasingeweza kuchukua makoloni mengi au kusambaza utamaduni wao duniani. Idadi kubwa ya watu iliwezesha ukuaji mkubwa wa kiuchumi kutokana na kuwekeza rasilimali watu katika viwanda na upanuzi wa miji, kuwa na walowezi katika makoloni waliyotawala, na kuwa na ushindi wa kijeshi na kibiashara.
Wakati huohuo Afrika ilikuwa katika hali mbaya wakati wa ukoloni kwa sababu watu walikuwa wachache sana na walioishi mbalimbali sana na walikuwa wamepoteza rasilimali kubwa ya watu kutokana na biashara ya watumwa. Kwa hiyo Waafrika wengi wakaondolewa kutoka Afrika na kusafirishwa kwenda nchi za Ulaya na Marekani ambako walitoa mchango mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi hizo. Na hapa ndipo tunapoona hasara za kuwa na idadi ndogo ya watu katika nchi:
Ndiyo maana iko hofu sasa kuwa ukuaji wa idadi ya watu barani Afrika inaweza kuwa kiashirio cha kupoteza nguvu kwa mataifa ya magharibi. Wakati mataifa ya Ulaya yakishuhudia kuporomoka kwa idadi ya watu wao, nchi za China na India tayari zina idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine yoyote duniani. Na Bara la Afrika litakuwa na nguvu kubwa kiuchumi na kisiasa kadiri ya idadi ya watu wake inavyoongezeka. Brian Clowes, Mkuu wa Idara ya Elimu na Utafiti wa Shirika la Kutetea Uhai duniani, Human Life International, katika makala yake “Population Control Agenda” anasema kuwa idadi ya watu Afrika mnamo 1950 ilikuwa asilimia 9 ya watu wote duniani, wakati Bara la Ulaya lilikuwa na watu asilimia 22 mwaka huo. Kufikia 1997 idadi ya watu wa Afrika na Ulaya ilikuwa sawa. Lakini mnamo 2050 idadi ya watu barani Afrika itakuwa asilimia 21 ya watu wote duniani, wakati idadi ya watu wa Ulaya itakuwa asilimia 8 tu. Takwimu hizo zinatoa maana kuwa, wakati idadi ya watu Barani Afrika inaongezeka kila mwaka, idadi ya watu Barani Ulaya inaendelea kupungua kila mwaka. Na kutokana na ukweli huo, Brian Clowes anasema kuwa programu za udhibiti wa idadi ya watu zinazoendelea sasa katika nchi zinazoendelea zina misingi ya kibaguzi.
Ndiyo maana sasa wanakimbilia kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu katika nchi zinazoendelea – wakati mwingine wakitumia mbinu chafu na danganyifu na hata pengine kutumia mabavu. Suala hilo sasa linaonekana kuwa ni hitaji la lazima linalopaswa kutekelezwa. Hayo yanatokana na ukweli kuwa watetezi wa programu za udhibiti wa ongezeko la watu wanafahamu fika kuwa kama idadi ya watu katika nchi zinazoendelea itaachwa ikue na wakati huohuo idadi ya watu katika nchi zao inaendelea kupungua basi itafika wakati nchi hizo zitatoa upinzani mkubwa katika medani za kisiasa, kiuchumi, kibiashara na kiustaarabu.
Hoja wanazozitoa kuhalalisha udhibiti wa idadi ya watu, kuwa eti ukuaji wa idadi ya watu katika nchi maskini kama ya kwetu kwamba unazuia kukua uchumi katika nchi hizo siyo za kweli. Hoja kama hii inatumika kwa hila kwa sababu watu wa magharibi wanafahamu uhusiano uliopo kati ya ukuaji wa idadi ya watu na kukua kwa maendeleo kwani watu ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi na maendeleo katika nchi.
MIKABALA TOFAUTI KATIKA PROGRAMU ZA IDADI YA WATU
Umoja wa Mataifa, kupitia Idara yake “Economic and Social Affairs”, kitengo cha Idadi ya Watu ukihitimisha taarifa yake kuhusu “Population Challenges and Development Goals” ya 2005 unaonyesha wasiwasi kuhusu mikinzano ya mienendo ya idadi ya watu katika nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Taarifa hiyo inasema kuwa nchi zilizoendelea na zinazoendelea zinatofautiana katika kuangalia masuala ya mienendo ya idadi ya watu.
Lakini kwa nchi zilizoendelea masuala yanayoumiza kichwa serikali zao ni viwango vya chini vya kizazi na madhara yake, ikiwa ni pamoja na
Masuluhisho ya kukabiliana na changamoto hizo yanatofautiana. Kwa nchi zilizoendelea suluhisho lake ni mwito wa kuongeza vizazi, yaani wanawake kuzaa watoto wengi. Suluhisho kwa nchi zinazoendelea linatolewa na serikali za nchi zile ambazo idadi yao inapukutika, nalo ni kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu.
Njia za kuongeza vizazi katika nchi zilizoendelea
Mnamo Novemba 1985, Jean Bourgeois-Pichat, Rais wa shirika moja lililojishughulisha na utafiti wa masuala ya idadi ya watu mjini Paris akizungumza katika kongamano kuhusu tofauti za kizazi alionyesha jinsi ndoa na uzao wa watoto ulivyokuwa ukiendelea kushuka katika nchi zote za viwanda na kutabiri kuwa pangekuwa na matokeo mabaya kwa idadi ya watu katika siku zijazo.
Muda mfupi baada ya Jacques Chirac kuchaguliwa kuwa Rais wa Ufaransa alionya, ‘kama unatazama Ulaya na katika nchi nyingine, ulinganifu wa idadi ya watu unatisha. Katika hali ya idadi ya watu, Ulaya inatoweka. Miaka 20 au zaidi kidogo baadaye nchi zetu zitakuwa tupu, hata kama tunao uwezo wa kiteknolojia tutashindwa kuitumia’. Naye Giscard d’Estaing aliyekuwa Rais wa Ufaransa kati ya 1974 hadi 1981 alionya wazi kuwa takwimu za sensa haziridhishi, kwani jamii inayoshindwa kujizalisha kizazi kingine ni jamii inayokufa.
Mnamo 1984 Bunge la Umoja wa Ulaya lilitoa azimio juu ya hitaji la kuchukua hatua katika kuhamasisha ukuaji wa idadi ya watu Barani Ulaya. Azimio hilo lilichukuliwa kwa kuzingatia kwamba umaarufu wa nafasi ya Ulaya duniani unategemea idadi kubwa ya watu, na kwamba idadi kubwa ya watu ni muhimu kwa maendeleo ya Ulaya na idadi kubwa ya watu itakuwa ndiyo kipimo kitakachoonyesha mchango utolewao na Ulaya duniani katika vizazi vijavyo
Uhamiaji ndio msingi wa ongezeko la watu katika nchi 27 za Umoja wa Ulaya. Katika kila watu wapya 10, 8 walikuwa wahamiaji. Asilimia 69 ya ukuaji wa idadi ya watu katika nchi hizo ilitokana na wahamiaji milioni 1.4; na asilimia 78 ya ongezeko la watu katika Nchi za Umoja wa Ulaya kati ya 1999 na 2008 ni matokeo ya uhamiaji; katika ongezeko la watu milioni 20.5, milioni 15,900,000 walikuwa wahamiaji.
Baada ya miaka mingi ya kuaminishwa kwamba uzao wa watoto wengi huleta umaskini, na wakiamini kwamba uzao wa mtoto mmoja au wawili ndio ishara ya maendeleo, wanawake wa Ulaya waliendelea kugomea kuzaa wakitumia vidhibiti mimba, utoaji mimba na hata kufunga kizazi. Utafiti uliofanywa na Taasisi inayojihusisha na masuala ya familia barani Ulaya, Institute for Family Policies, katika riporti yake ijulikanayo kama “Evolution of the Family in Europe 2009” umetoa taarifa kuwa, hatua iliyofuata ni kwa nchi za Ulaya kuamua kutoa motisha kwa familia kama njia ya kuhamasisha wanandoa kuzaa watoto wengi. Kulingana na sera za nchi husika, kila familia hulipwa na serikali kiasi fulani cha fedha kila mwezi ili kuhamasisha kuzaa watoto wengi. Kiasi cha malipo huongezeka kila mwaka.
NCHI | Familia zenze watoto 2 | Familia zenye watoto 3 |
Luxembourg | Euro 471 | Euro 833 |
Ireland | 332 | 535 |
Ujerumani | 328 | 498 |
Austria | 293 | 510 |
Denmark | 266 | 398 |
Ubelgiji | 362 | 497 |
Serikali hutoa fedha kwa ajili ya kugharamia sehemu ya matunzo ya watoto wanaozaliwa katika familia. Fedha hizo hutolewa kwa kila mtoto azaliwaye bila kuwa na ukomo. Angalia mfano huu na fedha zinazotolewa [Euro]:
NCHI | Mtoto 1 | Watoto 2 | Watoto 3 | Watoto 4 | Ukomo |
Luxembourg | 216 | 255 | 362 | 392 | Hakuna |
Ireland | 166 | 166 | 203 | 203 | Hakuna |
Germany | 164 | 164 | 170 | 195 | Hakuna |
Austria | 140 | 154 | 217 | 195 | Hakuna |
Denmark | 133 | 133 | 133 | 133 | Hakuna |
Belgium | 104 | 159 | 235 | 235 | Hakuna |
Finland | 100 | 111 | 141 | 182 | Hakuna |
Sweden | 97 | 106 | 130 | 176 | Hakuna |
Netherlands | 80 | 88 | 88 | 97 | Hakuna |
France | - | 145 | 224 | 245 | Hakuna |
United Kingdom | 85 | 57 | 57 | 57 | Hakuna |
Cyprus | 40 | 53 | 170 | 292 | Hakuna |
Mnamo 2008 mafao kwa watoto yaliongezeka kwa wastani wa asilimia 5.3
Wastani wa likizo ya uzazi ni majuma 25.3. Nchi zenye likizo ndefu za uzazi ni Sweden (majuma 75.7), Bulgaria (majuma 58.6), United Kingdom (majuma 52) na Denmark (majuma 50). Inasemekana kuwa upo uhusiano kati ya mafao ya kifedha kwa watoto wazaliwao na kumalizika kwa umaskini. Kwa kadiri watoto wanavyolipiwa mafao makubwa ya kifedha na serikali ndivyo hivyo inavyokuwa vigumu watoto hao kuwa maskini.
Kuhuisha vizazi kwa kuzipatia familia mazingira bora ya kuishi na kuzaliana
Kuihuisha familia kama taasisi inayoheshimika na kutegemewa
HILA KATIKA SULUHISHO LA MASUALA YA IDADI YA WATU KATIKA NCHI ZINAZOENDELEA
Ushawishi, mabavu na shurti
Jitihada zilizochukuliwa katika kukabiliana na kuporomoka kwa vizazi katika Bara la Ulaya hazijafaulu kuwafanya watu wazaliane na hivyo kuepusha nchi hizo kuwa ‘tupu’ katika miaka ijayo, washukuru kuna wimbi kubwa la wahamiaji, la sivyo hali yao ingekuwa mbaya zaidi. Suala linalowasumbua kwa muda mrefu hili, ‘je, watafanyaje kudhibiti ukuaji wa idadi ya watu katika nchi maskini ili zisiinukie dhidi yao’? Tangu miaka ya 1960, bila kuweka mipango hiyo bayana, nchi za Magharibi zilianza mikakati ya kudhibiti ukuaji idadi ya watu katika nchi maskini na zinazoendelea zikitumia lugha nzuri ya ‘uzazi wa mpango’. Na suala la uzazi wa mpango lilihusishwa na misaada ya maendeleo. Ikazalishwa propaganda kwamba ongezeko kubwa la idadi ya watu linazuia ukuaji wa maendeleo na hivyo katika kupokea misaada nchi maskini na zinazoendelea zililazimika kuweka programu za kupunguza ukuaji wa idadi ya watu katika mipango yote ya maendeleo. Na katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na shirika la Population Council mapema 1991 ilikadiriwa kuwa tayari uzao wa watu milioni 412 umezuiwa katika nchi hizo kwa kutumia programu za uzazi wa mpango uliofadhiliwa na kutekelezwa na nchi tajiri.
Elizabeth Liagin, katika makala iliyochapishwa katika www.africa2000.com yenye kichwa cha habari “Differential Fertility: Western Anxieties about Population Decline” anasema kuwa, ingawaje kupungua huko kwa vizazi kulitokana na uamuzi wa hiari wa kupanga uzazi, upo ushahidi wa kutosha unaoonyesha kwamba kulikuwa na programu za makusudi za kiuchumi na kijamii zilizoratibiwa zenye kupendelea kudhibiti uzao, palikuwa pia na propaganda, maelekezo kutoka wahudumu wa afya na viongozi wa kiserikali na kisiasa, udanganyifu, kulazimishwa na hata matumizi ya nguvu. Vilevile vivutio vya kifedha, nguo, au vinginevyo vilitumika kuwalazimisha watu kuingia kwenye programu za kufunga kizazi, kama ilivyokuwa huko Bangladesh miaka ya 1970 katika programu ilijulikana kama “Green Star” ambayo hapa kwetu tumeipa jina “Nyota ya Kijani”.
Huko India shirika la kimataifa linalojishughulisha na uzazi wa mpango na utoaji mimba, “International Planned Parenthood Federation” linasimujia jinsi wanawawe walioamua kufunga kizazi walivyozawadiwa nazi, vyombo vya nyumbani, na kuchukuliwa kama mfano wa kuigwa. Wale ambao hawapendi kufungwa kizazi wanashawishiwa, na pengine maneno ya kejeli yanatumika dhidi yao, ‘mawazo mgando’, ‘kushikilia mila potofu’, ‘kupitwa na wakati’, ‘ubabe’, ‘unyanyapaa’ na maneno au misemo mingine mingi.
Katika makala iliyondikwa na Penny Starr, Januari 12, 2012 na kutolewa na CNSNews.com, katika mpango mkakati wake wa 2010-2015 shirika la International Planned Parenthood Federation [IPPF] limedhamiria kuongeza huduma za utoaji mimba Barani Afrika kufikia asilia 82. Katika mkakati huo, IPPF imedhamiria kupigania programu za ‘utoaji mimba salama’, ikiwa ni pamoja na utoaji mimba wa kikemikali [kwa kutumia vidonge], na utoaji mimba mahospitalini na katika zahanati na huduma za uzazi wa mpango baada ya mimba kutoka [post abortion care].
Programu za udhibiti wa ukuaji wa idadi ya watu hupitia hatua mbalimbali katika utekelezaji wake. Mwanzoni programu hizo hazionyeshi kuwa na madhara kwani watu wanaaminishwa kwamba, uzazi wa mpango huleta faida katika maendeleo ya nchi. Vijana hupewa udhamini wa kielimu ili wakajifunze nje ya nchi zao faida za uzazi wa mpango na wanaporejea makwao wanakuwa ndio wahamasishaji wakuu, wakitumia vyombo vya habari, semina, warsha, mikutano, makongamano na njia nyingine za kuwasadikisha watu. Kwa kawaida programu hizo huendana na malipo makubwa ya kifedha kama motisha kwa wahudumu wake. Hatua inayofuata ni wafadhili kulipia huduma za uzazi wa mpango katika ngazi za msingi – jumuiya, zahanati. Halafu wafadhili au wadau wa maendeleo, na pengine nchi hisani wanaanza kushirikiana na serikali za nchi husika ili kutengeneza sera zenye kupendelea uzazi wa mpango na misaada hutolewa kwa ajili hiyo.
Serikali ikikubali kushiriki katika programu hiyo, basi ufadhili huwa mkubwa na programu mbalimbali hutengenezwa kwa ajili ya utekelezaji. Ufadhili hutolewa hata katika shughuli za kimaendeleo kama motisha kwa serikali husika, kwa mfano, ufadhili unaweza kuwemo katika misaada ya kimaendeleo katika kilimo, kwa vijana, yatima, walemavu, na hata kuvipatia fedha vyama vya siasa ili kujenga utashi wa kisiasa. Ushiriki wa viongozi wa kisiasa na kiserikali ni muhimu katika kufanikisha programu hizi. Kwa kawaida, hatua hii ikifikiwa, huduma za ‘uzazi wa mpango’ huwa za kitaifa, na uhamasishaji au hata ulazimishwaji hufanyika katika ngazi zote za serikali. Watendaji katika vijiji huwa ndio mawakala wakuu wa programu hizo. Watendaji kutoka ngazi za juu wakiambatana na ‘wafadhili’, ambao pia wanajulikana kama ‘wadau wa maendeleo’, hutembelea vijiji na kuongea na viongozi wa vijiji hivyo. Halafu wanakijiji huitwa katika mkutano ya hadhara na kuelezwa faida za ‘uzazi wa mapngo’ na hatua za kuchukua, kama ni kufunga kizazi, kutumia vidonge, sindano, vipandikizi, vitanzi, au njia nyinginezo.
Sera za elimu huingiza masuala ya uzazi wa mpango na mitaala ya hubadilishwa ili kuongeza masomo ya uzazi wa mpango kuanzia ngazi ya elimu ya msingi. Katika ufundishaji faida za uzazi wa mpango huelezwa kwa watoto kama ilivyoandikwa katika kitabu: Sayansi kwa Vitendo – 7; Kitabu cha Mwanafunzi, Muhutasri wa 2005, kilichotolewa na Mture Educational Publishers Limited, Dar es Salaam na kupatiwa cheti cha Ithibati na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mei 23, 2011 ili kitumike kwa wanafunzi wa darasa la saba.
Katika huduma za kliniki wahudumu wameelekezwa kuwakatisha tamaa wanawake wenye uzao wa watoto zaidi ya wawili, na kwa kweli katika kliniki nyingine, wahudumu wanawakemea wanawake waliozaa watoto wanne au zaidi. Tumesikia pia wanawake wakilalamika kuwa wameelezwa na wahudumu kule kliniki kuwa wasirudi tena hadi ipite miaka mitano. Mtu mmoja alinipigia simu kutaka kufahamu kama kuna kliniki nzuri ili ampeleke mke wake aliyekuwa mja mzito. Nilipomwuliza sababu za uamuzi huo alinieleza kuwa mke wake amekuwa akipata manyanyaso anapohudhuria kliniki katika vituo vya serikali. Aliendelea kunifahamisha kuwa huko alikuwa anatukanwa, kubezwa na hata kufokewa kwa vile tayari alikuwa amezaa watoto wanne. Hivi majuzi tu nilimpeleka mama hospitali fulani kwa matibabu. Wakati nasubiri huduma nilimtuma Grace Shayo, Katibu wangu Muhutasi, ajipenyeza katika kliniki ya hospitali hiyo na akabahatika kuwa mmoja wa waliopta maelezo juu ya faida za uzazi wa mpango. Lakini kilichomshangaza ni kushuhudia idadi kubwa ya akina mama waliokuwa wanalalamika juu ya madhara waliyopata baada ya kutumia huduma hizo. Kila aliyenyosha mkono kutaka kuongea, alieleza masikitiko yake jinsi alivyoumizwa na vidhibiti mimba. Yule mshauri nasaha aliwashauri kubadilisha njia, yaani kama walitumia vidonge, basi watumie sindano, na kama mmoja alitumia sindano, basi atumie vipandikizi au vidonge. Kwa bahati mbaya akina mama walishuhudia kuwa vidonge, sindano, vipandikizi na vitanzi vyote vilikuwa na madhara makubwa katika afya zao. Mhamasishaji hakukata tamaa, aliendelea kuhamasisha ili wanawake waendelee kutumia njia hizo licha ya malalamiko ya akina mama wale.
Mnamo 1992, jarida la “Clearinghouse Bulletin” likiandika katika ukurasa wake wa kwanza lilisema, kuna muda wa kusubiri watu wakubali kwa hiari kutumia vidhibiti mimba, na liliorodhesha vivutio vingi vya kuwafanya watu wakubali kwa hiari yao, na hata vitisho kwa wale watu wenye familia kubwa ambao wangekataa. Kimsingi, jitihada zilifanyika za kueleza hasara za kuwa na watoto wengi katika familia – ‘hali ngumu ya maisha’, ‘huduma za elimu’, matibabu, chakula, mavazi, n.k. Hatimaye jarida lilisema, kama ‘vivutio’ na ‘vitisho’ vinavyofanikisha uzao wa watoto wawili vinawekwa. Hatua ya mwisho ni ile ya kutumia nguvu, yaani kutumia programu za mabavu katika kuwalazimisha watu kufunga kizazi. Yaliyoandikwa katika jarida hilo ndiyo yanayofanyika sasa hapa Tanzania. Katika kitabu Sayansi kwa Vitendo - 7; Kitabu cha Mwanafunzi, Muhutasari wa 2005; kilichotolewa na Mture Educational Publishers Limited, Dar es Salaam, (ambacho kimeandikwa “Hakiuzwi: Ni Mali ya Serikali ya Tanzania”) kinaorodhesha hasara za kutopanga uzazi kama:
Ni katika mtazamo huo, Melinda Gates akishirikiana na Serikali ya Uingereza aliandaa mkutano wa matumizi ya vidhibiti mimba kwa watu wa nchi maskini duniani, akiamini eti kuwapa wanawake uwezo, kupunguza umaskini na kuimarisha afya za wanawake ni malengo mazuri. Melinda Gates anadai kwamba ufunguo wa kuondoa umaskini katika nchi maskini na zile zinazoendelea ni kuhamasisha na kusambaza matumizi makubwa ya vidhibiti mimba. Anaamini kwamba jitihada zake zitawafikia wanawake milioni 120 duniani, akiweka mkazo katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na Kusini mwa Asia. Kwa upande mwingine, watafiti wa masuala ya idadi ya watu wanasema, suluhisho hili la Melinda Gates litaleta vifo visivyohesabika vya watoto ambao bado hawajazaliwa, inaweza kufanya ongezeko la virusi vya ukimwi kuwa mara dufu na inaweza kuongeza uwezekano wa saratani ya matiti. Zaidi ya hapo vidhibiti mimba vyenye chachu ya projestini tu vinahusika na kuongeza uwezekano wa kuganda damu na kiharusi.
Lakini kwa nini Bill na Melinda Gates kupitia shirika lao, “Gates Foundation” wajihusishe na masuluhisho ya hila kwa kisingizio cha kuondoa umaskini katika nchi zinazoendelea”?. Jibu lake limo katika malengo yao ambapo wanaamini kuwa kufikia 2050 idadi ya watu duniani inategemea kufikia bilioni 9, ambalo ni ongezeko la asilimia 50 kutoka 2005. Ongezeko hili;
Wanasema kuwa uzazi wa mpango ndio njia bora zaidi ya uwekezaji katika nchi maskini kwa vizazi vijavyo.
Wachambuzi wa masuala ya idadi ya watu wanasema kuwa jitihada hizi ni marejeo ya nadharia za Malthus ambazo zimetumika tangu karne ya kumi na tisa. Wasiwasi kuhusu ukuaji wa idadi ya watu hupelekea kuanzisha jitihada za kudhibiti kizazi cha watu wanaosemekana kuwa hawafai. Mwanzilishi wa shirika la Planned Parenthood, Margaret Sanger alisukumiza matumizi ya vidhibiti mimba [na utoaji mimba] kwa watu weusi wa Marekani kama njia ya kudhibiti kuongezeka kwao. Na sasa Bill na Melinda Gates wanaona matumizi ya vidhibiti mimba kama njia bora ya kudhibiti ongezeko la watu wa Afrika na Asia ya Kusini.
Melinda Gates na washirika wake, ikiwemo Serikali ya Uingereza na mashirika makubwa duniani yanayopigania kutungwa sheria za kutoa mimba wamezindua kampeni ya kukusanya dola za Kimarekani bilioni 4 ili kusukuma matumizi ya vidhibiti mimba kwa wanawake maskini wa nchi za Afrika, Asia na Amerika ya Kusini.
Angalia video katika mtandao huu
https://www.youtube.com/watch?v=IuitL4XhDAA
SULUHISHO LA KWELI KATIKA KUONDOA UMASKINI
ndivyo vitatuwezesha kusonga mbele kimaendeleo