Leo tunajadili umuhimu wa tumbo lamama kama mahali pekee ambapo Mungu alipachagua kuwamakazi yamuda ya mtoto mchanga kabla hajazaliwa. Tunataka kutafakari leo na kuwauliza akina mama wa leo, jee, matumbo yao yamekuwa mahali salama kwa makazi ya watoto? Lakini tunatafakari pia jinsi Mungu alivyomtayarisha kila mtoto kwa huduma, utumishi au madaraka katika uhai wake baada ya kuzaliwa na kukua. Lakini tunataka kuwatoa wasiwasi wanawake wote kuwa hicho kilichomo ndani ya tumbo lako, au hicho kinachoitwa mimba ni binadamu mdogo, mwenye akili na mwenye kujimudu katika hatua yake ya kukua. Kwa hiyo kitendo chochote cha kumwua mtoto aliyemo ndani ya tumbo la mama katika kile kinachoitwa utoaji mimba, ni mauaji ya binadamu mdogo ambaye anakuwa na kwamba baada ya kumwua hakuna binadamu mwigine anayechukua mbadala wake, anakuwa amepotea moja kwa moja na hatutamwona tenda kwa macho, tukamshika, tukambembeleza.
Mungu hutumia tumbo la mwanamke kuleta uhai mpya duniani; wito wa kuheshimu na kutunza mimba; kila binadamu ni wa pekee na kila binadamu analetwa duniani kutimiza matakwa fulani ya Mungu; hakuna binadamu aliyeumbwa na Mungu asiyekuwa na faida.
Mwa. 16:11-12 - uzao wa Ishmael
Mwa. 25:21-26 - uzao wa Esau na Yakobo
Kut. 21:22-25 - wito wa kuheshimu na kutunza mimba
Isa. 21:14- utabiri wa uzao wa Yesu
Isa. 44:1-2;24- wito wa kuwa mkombozi wa Waisraeli
Isa. 46:3-5- Mungu mkombozi wa Israeli
Isa. 49:1-3- wito wa Unabii wa mtumishi wa Bwana
Ayu. 3:!3-15- ni vibaya kuua kabla au wakati wa kuzaa
Ayu. 10:8-12- uumbaji kudhihirisha ukuu na huruma ya Mungu
Ayu. 31:15- umuhimu wa kuwahudumia wengine
Zab. 22:9-11- uumbaji na ukuu wa Mungu
Zab. 139:13-16- ni Mungu pekee mwenye ufahamu wa binadamu
Mhu. 5:14-15; 11:5- binadamu si chochote mbele ya Mungu
Mat. 1:18-21- uzao wa Yesu na ukombozi wa binadamu
Luk. 1:13-15- uzao wa Yohane
Luk.1:36.39-44- kutano la Elizabeti na Maria: uhai wa mtoto
Mafundisho kutokana na sehemu hizo za maandiko
Kila mama mja mzito hubeba uhai wa binadamu kamili tumboni mwake
Kila mtoto katika tumbo la mama ni wa pekee na asiyeweza kujirudia
Kila mama anabeba Baraka ya Mungu kwa kuwa mshiriki wa uumbaji pamoja na Mungu; hivyo kila mama mja mzito ni MBARIKIWA WA MUNGU
Kila binadamu amepangiwa na Mungu majukumu yake hapa duniani tangu akiwa tumboni mwa mama yake
Ni wajibu wa kila mama kuitunza mimba yake na kuilinda dhidi ya mashambulio yoyote yale
Ni Mungu pekee mwenye kumjua kila binadamu kwa undani jinsi alivyo kutokana na tendo lake la uumbaji [soma Zab. 8:5-6]
Tendo lolote la kutoa mimba ni tendo la kuua mtoto anayekua tumboni mwa mama na aliyeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu na aliyeshirikisha pande tatu: Mungu, mwanaume na mwanamke
Kila mwanamke anayetoa mimba anamuua mtoto wake mwenyewe, anaiua sehemu ya nafsi yake na anabeba laana na kuondoa ubarikio wa Mungu
Kila binadamu na amshukuru Mungu kwa kuumbwa kwa jinsi ya ajabu ya kutisha
Kila binadamu ni tunda la fikra ya Mungu [soma Mwa. 1:26] na hivyo kila binadamu anashiriki u-takatifu wa Kimungu kwa njia ya pumzi hai ya Mungu isiyokufa, ndiyo roho yake