TANZANIA INAYO HAKI YA KUKATAA SHERIA YA UTOAJI MIMBA
TANZANIA INAYO HAKI YA KUKATAA SHERIA YA UTOAJI MIMBA
1. Kuhalalisha utoaji mimba kwa namna yoyote ile au sababu yoyote ile ni kuhalalisha mauaji ya halaiki “Genocide” kwa vizazi vijavyo na vya sasa.
2. Kushinikiza kipitisha sheria ya namna hiyo ambayo wenzetu wa Magharibi na Mashariki wameipitisha lakini wakashindwa kuifuata kwa sababu ya madhara yake ni kuwa vipofu wa maarifa.
3. Tanzania tunayo kila sababu na nia ya kukataa sheria ya namna hiyo hata kama mataifa yote duniani yatakuwa yameipitisha sheria hiyo kwao.
(i)Tanzania ni nchi ya uhifadhi wa mazingira na viumbe hai.
(ii)Historia inatuambia hata binadamu wa kwanza alianzia Tanzania Kondoa Irangi.Hivyo Tanzania iwe Taifa la hifadhi ya kizazi cha binadamu (Human Ecology) na urithi wa dunia.
4. Tanzania tunayo mila na desturi ambayo huheshimu uhai wa binadamu tangu mimba inapotunga. Mimba iliyoharibika kwa bahati mbaya kama ni mume au mke hutakiwa kufanyiwa tambiko zote za kifamilia na ukoo kumtambua kama mmoja wa ukoo anayestahili heshima zote.
Tanzania tunazo dini mbalimbali ambazo ni UKRISTO na UISLAMU, UBUDHA na UHINDU hizi huhifadhi sana uhai wa binadamu tangu mimbani.
1. Kwa mfano ukristo: Mwanzo 1:26-28
Mwanzo 2:7
Mwanzo 3:15
Jeremia 1:5
2. Uislamu: Koran 133-“Yeyote aokoaye maisha ya mtu mmoja huhesabiwa kuokoa taifa lote”.
Yeyote auaye mtu mmoja isipokuwa kwa mambo ya sheria huhesabiwa kuwauwa wanadamu wote.
Uislamu: Koran 6:151- Usiue au usitoe uhai wa mwanadamu ambae mwenyezi Mungu aliuita kitakatifu (Sacred).
Dini nyingine ni kama Buddhism – Kwa dini ya Wabudha utoaji mimba ni uuwaji na ni uovu mbaya wa kusumisha uhai wa binadamu ( Clive Erricker Holdder and strongton1995(119).
Wakristu (Juda Christian Traditon) Biblia takatifu humtambua mwanadamu na kumheshimu kabla ya kuzaliwa.
Jeremia 1:5 “Kabla sijakuumba ndani ya tumbo nalikujua kabla hujazaliwa nalikutakasa uwe nabii wa mataifa.
Luka 1:41, Zaburi ya 139 inaeleza jinsi mtoto akuavyo tumboni mwa mama yake.
Mafundisho ya mitume 12 (Didache) yanasema, usimuuwe mtoto tumboni mwa mama yake. Madhehebu ya protestant na yote ya kikristu (eg Ireland ya Kaskazini) Wakatoliki na Waprotestant wameungana kupinga utoaji mimba.
Wahindi: wahindi huita (abortion) utoaji mimba “Garha-batta” mauaji ndani ya tumbo la uzazi na “Adhara veda” inelezea mtoaji mimba (abortionist) kama mkuu wa wadhambi wote.
Mahatma “Ganddhi mhindu” aliyeheshimiwa sana karne ya 20, alisema “inaonekana kwangu katika mwanga kama mwanga wa mchana, kwa hakika utoaji mimba ni uovu mkumbwa sana”
Waisraeli (Judaism) torah (sheria ya kiisraeli inakataza mauaji ya asiye na hatia na kusisitiza kwamba wanadamu wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Maimonida mfasiri wa sheria ya kiisrael alisema “yeyote aliyetokana na kizazi cha Noah akiuwa mtu hata kichunga mimbani (fetus) kwenye tumbo la mama auwawe).
Lakini swali la kujiuliza ni je! Mtoto aliyemimbani ni mwanadamu? Au (is the fetus a member of the biological species (i.e homosapiens) (a human being?)
Kujibu swali hilo tuwaombe wanasayansi ya DNA (tunajua baada tu ya utungaji kiumbe chromosome 23 za baba na chromosome 23 za mama huungana na kufanya kiumbe kipya tofauti na wazazi wote wawili ni pekee ambaye hafanani na yeyote aliyekwisha umbwa na hawezi kurudiwa tena. (Unique and unrepeatable).
Hivyo kuua mwanadamu asiye na hatia ni uovu mkubwa hata kwa yeyote asiyeamini
au asiye na dini yoyote. Kwa mantiki hiyo sisi watanzania tusimame kidete tusifanye makosa waliyokwisha fanya wenzetu.
Wengine husema mimba itolewe kwa ajili ya kuokoa maisha ya mama na kusahau kwamba kwa kufanya hivyo mtoto huhukumiwa kifo bila kujitetea na hii ni kinyume na haki za kibinadamu; haki ya kwanza msingi ikiwa ni uhai au haki ya kuishi. Kila mtu anayo haki ya kujitetea mbele ya sheria na kuonekana na hatia ndipo ahukumiwe. Mtoto mimbani atapewa lini nafasi hiyo?
Kuhalalisha utoaji mimba ni kujiondoa katika mataifa yaliyo staarabika duniani nakurudia kua taifa duni kimaarifa (primitive nation)
Serikali ikifanya hivyo imejitwalia uweza wa kimungu hivyo tutakuwa taifa lililomwasi muumba wake.mwanzo 2: … “yeyote atakayemuua Kaini atalipizwa kisasi mara saba” maneno na mafundisho ya Yesu waacheni watoto waje kwangu “yeyote ampokeaye mtoto mdogo kama huyu anipokea mimi”
Wataalamu ambao hushughulikia uhai kama Madaktari na Wauguzi kwa kiapo wapewacho cha kulinda uhai wa wanadamu tangu saa ile mbegu na kijiyai vinapoungana, Sheria ya namna hiyo ikipitishwa wote itabidi waache kazi au kiapo chao kibadilishwe ili waruhusiwe kukiuka kiapo chao hicho na watakapobadilika moja kwa moja tuache kuwaita Madaktari au wauguzi wapewe jina lingine la “WACHINJAJI” na hospitali zetu na zahanati zitakuwa mabucha ya kutuchinja wanadamu.
Kwa sheria ya namna hiyo Watanzania wote tutakuwa tumejitayarishia mfumo usio na usalama wowote (Pro-life).
Hitimisho
The bill to inact safe motherhood law 2012
Termination of pregnancy (utoaji mimba)
Ndugu wasikilizaji hebu tusikie sheria inavyopendekeza utoaji mimba na mwenye mamlaka ya kutoa hiyo mimba inasema:Je 17 1 (A) mimba inaweza kutoelewa
Kama mhudumu wa afya kwa kushauriana na mama mjamzito wana maoni kwamba
Mimba ikiendelea inaweza kusabisha hatari au jeraha kwa mwanamke kimaumbile au kiakili.
Kuna wasiwasi kwamba mototo aliye mimbani anaweza kupata jeraha la kimwili au kiakili
Mimba imesababishwa na ndugu wa karibu (kama baba mzazi, mjomba, kaka au amebakwa).
Huyu mama mjamzito kwa sababu ya kuwa kiakili ameathirika hana uwezo wa kukubali hiyo mimba.
Ndugu watanzania sababu zilizotajwa na sheria hii zina uzito wowote unaosababisha kuwauwa watoto wachanga mimbani? Inaonekana wanapendekeza jambo hilo ni mumiani wanaotamani sana damu na nyama ya vichanga vya Watanzania.
Kwa jinsi technologia ya sayansi ya matibabu ilivyoendelea hakuna hata sababu moja ambayo technologia hiyo itashindwa kutibu mama mjamzito na mtoto wake mwenyewe hata isababishe mtoto aliye mimbani ahukumiwe kifo ili kumwokoa mama yake. Mimi ambaye nimewahudumia wanawake ilikua kifafa cha mimba ni hatari sana kwa wote mama na mtoto lakini siku hizi kifafa cha mimba hutibiwa kwa dawa na mama pamoja na mtoto huwa salama wakati wa ujauzito
17 1 (A)
2. Utoaji mimba unaweza kufanywa tuu na mhudumu wa afya aliyefunzwa na kupewa cheti kwa sababu hiyo serikali kwa kujua fika jambo hilo halitakubaliwa
Kufanywa na madaktari na wauguzi imetafuta njia mbadala ya kutoa cheti kwa
mtu yeyote ambaye amepewa mafunzo hata ya siku moja kufanya uchinjaji wa watoto wetu walio mimbani?
3. Utoaji mimba kwa njia ya upasuaji inaweza kufanywa kwenye kituo cha huduma kilicho teuliwa na Waziri kwa kutoa taarifa tuu kwenye gazeti la serikali? Niulize hivyo vituo teule siyo hizo hospitali zetu na zahanati, hivyo wanakwepa kwani hospitali na zahanati zilizopo hazitakubali kufanya mambo ya kishetani namna hiyo.
4. Waziri anaweza kuteua kituo cha kutolea huduma hiyo iliyotajwa kifungu cha 1 mradi tuu matakwa ya utoaji mimba yatekelezwe. Hivi huyo Waziri au ni Mbunge na mjumbe wa baraza la Mawaziri wa Serikali yetu tukufu?kazi kwetu Watanzania.
5. Waziri anaweza kuondoa kibali kwa kituo chochote teule baada ya kutoa taarifa ya siku 14 na kuondoa uteuzi kwenda gazeti la Serikali?
(18) Taifa litakuza na kuhimiza ushauri nasaha ambao si wa lazima na ushauri nasaha usio elekezi kabla na baada ya utoaji mimba. Hivi ushauri nasaha usio muhimu na usio elekezi una maana gani? Kwamba kusiwepo na ushauri wowote ambao utamfanya mjamzito akatae utoaji mimba.
(19) Inatumika tu katika lugha danganyishi ya sheria kwamba kIfungu cha 17 (1) kwamba kabla ya kutoa mimba kuwa na ushauri nasaha juu ya madhara ya utoaji mimba.
(20)1. Wizara itahakikisha vituo vya afya vitazuia na kutibu madhara yatokanayo na utoaji mimba holela kwa bajeti gani?Kwani hata dawa za Malaria ni shida?
(20) 2. Mhudumu yeyote wa afya anayekiuka vifungu 17,19 na 20 atakua ametenda kosa la jinai na akikutwa na hatia hiyo atatozwa fine ya sh.500,000 au kifungo miezi 6 au vyote.
Hivi hao wahudumu si sisi Madaktari na wauguzi ambao hatutakubaliana na mambo ya kiupuuzi na ovyo hivyo katika taifa letu.
Tunawaomba hawa vibaraka walioshiriki kuandaa mswada huu waadhibiwe kikamilifu na jamii na hiyo serikali itakayokubali upuuzi huo ianze kuondoka madarakani kabla Watanzania hawajachukua hatua kali za kinidhamu.