Ni chachu bandia ya projestini iliyotengenezwa katika maabara ambayo mwanamke hudungwa mg 150 kila baada ya miezi mitatu. Chachu hii bandia huitwa Depot - MetroxyProgesterone Acetate {DMPA}. Depo provera ambayo tumezoea kuita sindano ya Depo Provera ambayo hadi 1996 ilitumiwa na wanawake milioni 30 katika zaidi ya nchi 90 duniani, nyingi zikiwa nchi maskini, inaaminika kuzuia mimba kwa miezi mitatu. Dawa hii ilithibitishwa kwa matumizi huko Marekani mwaka 1992. Lakini mwezi Juni 1993 Idara ya Afya ya Kanada ilizuia matumizi ya dawa hiyo kwa maelezo kuwa sio salama kwa afya ya watumiaji. Ili kuepusha madhara kwa wanawake wa Ulaya, Shirika la Afya Duniani lilifanya majaribio ya dawa hii kwa wanawake wa nchi zinazoendelea, kama vile Kenya, Mexico, Thailand na New Zealand.
3. Utendaji wake
Kwa kadiri ya jarida la ‘‘Upjohn’’ Depo Provera depo provera huzuia utoaji chachu zinazohitajika kwa ajili ya kuivisha yai. Hali hiyo husababisha ngozi nyororo katika mji wa mimba kuwa laini na hivyo kushindwa kumpokea bindamu mpya. Vile vile inabadilisha ute na kuwa mzito na kuzuia mbegu kupenya kwa urahisi kuelekea tumbo la uzazi na mirija yake. Depo provera ni kiua mimba. Wanawake wengi wanaotumia depo provera hupata hedhi asilimia 43 baada ya miezi 12 na silimia 32 baada ya miezi 24. Takwimu hii inatusaidia kufahamu kuwa sio katika wanawake wote dawi hii hufanya kazi kwa kiwango kile kile.
4. Je depo provera ni salama ?
Huko Marekani Shirika la Chakula na Madawa lilikataa kuthibitisha matumizi ya dawa hiyo kwa miaka 20 tangu 1972 hadi 1992. Baadhi ya sababu ni :-
Baadhi ya watetezi wa dawa hii, ambao walilishinikiza Shirika la Chakula na Madawa la Marekani kuipitisha walikuwa wanajihusisha na masuala ya udhibiti wa idadi ya watu duniani.
Wakati wa majaribio kwa wanyama, ilionekana kusababisha uvimbe wa matiti kwa mbwa na saratani ya tumbo la uzazi kwa nyani.
Dawa yoyote inayoleta madhara kwa wanyama, kuwa hivyo pia kwa binadamu.
Dawa hii ilionekana kusababisha saratani ya mlango wa tumbo la kizazi kama ilivyoripotiwa na msemaji katika Taasisi ya Taifa ya Saratani huko Marekani.
Dawa hii ilishinikizwa kwa watu weusi (Negro) na Wahindi huko Marekani, na katika nchi zinazoendelea. Vile vile dawa hii inatolewa kwa watu wasio na elimu, wenye mtindio wa ubongo, na kutolewa kwa siri kwa makundi ya vijana. Utafiti uliofanyika kufuatia jambo hili, ulionyesha madhara makubwa kwa watumiaji hasa uvimbe katika matiti yao.
Ufafiti uliofanywa na Jarida la habari la « Upjohn » kwa miaka 11 huko Atlanta kwa watu weusi waliotumia dawa hiyo, ulionyesha kuwa ; baadhi ya wanawake walikufa, wengine walipata saratani, wengine dawa iliwajengea muelekeo wa kujiua kutokana na mgandamizo wa moyo .
Katika miaka ya 1990 baadhi ya nchi kama vile Canada na India zilizuia matumizi ya Depo provera, kutokana na madhara yaliyowapata wanawake.
Shirika la chakula na dawa la Marekani, lililazimisha kampuni ya Frizer kubandika tangazo lenye tahadhari kuwa inaleta madhara ya kutisha, kama vile, kupoteza madini kwenye mifupa. (Osteoporosis)
Madhara zaidi ya depo provera
Mabadiliko ya hedhi, kutoka damu nyingi na kwa muda mrefu (anemia), kutoka damu nzito, kutoka damu kidogo, kutotoka damu kabisa, damu kidogo, kutoka damu matone matone na kutoka damu bila mpangilio.
Kuongezeka uzito na uzito huo huongezeka kadiri ya muda wa matumizi na aina ya mtumiaji (kila 1 hadi 5 kila mwaka) .
Kupoteza uzito katika mifupa (osteoporosis)
Maumivu ya magoti
Kupungua uwezo wa kupokea sukari.
Wasichana wengi walio chini ya umri wa miaka 35 huwa na uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya matiti.
Mabaka mabaka
Saratani ya mlango wa kizazi
Kupasuka kwa mishipa ya damu kutokana na kuziba kwa mshipa mkubwa na kuganda damu / hewa.
Kuziba kwa mshipa mkubwa na kuganda damu/ hewa
Matatizo ya akili
Upofu wa macho
Kuzaa mtoto mwenye vidole zaidi ya kawaida au walioungana.
Kuwa na wasiwasi, kutotulia
Kujaa maji mwilini
Kichefuchefu
Ugonjwa wa manjano
Kifafa cha mimba
Uvimbe katika uke
Kupooza
Tafiti nyingine zilizofanywa zimesema kuwa wanawake wanaotumia depo provera wana hatari ya kupata magonjwa ya zinaa kama vile Clamdiya, Gonorrohea, Herpes Virus mara tatu zaidi ya kawaida.
50% ya wanaopata mimba, hali wakitumia Depo provera wana uwezekano wa kuzaa watoto njiti.
90% , kama wanaacha Depo provera wiki 4, baadaye wakipata mimba wanazaa njiti.
80% ya watoto wanaozaliwa ambao walitungwa mimba mama yao akitumia au mara tu baada ya kuacha
29. Kuchelewa kupata mimba au kutopata mimba kabisa.