4. Mungu hutumia tumbo la mwanamke katika kuleta uhai mpya wa binadamu
Mwa.16:11; 25:21-26
Kut. 21:22
Isa. 7:14; 44:2, 24; 46:3; 49:1, 2; 53:6
Ayu.3:11-16; 10:8-12; 31:15
Zab. 22:9-10; 139:13-16?
Mhu. 5:15; 11:5
Luk. 1:13-15;1:36, 39-44
Mt. 1:18
Kwa sababu hiyo tuna kila sababu ya kukiri kwamba tumbo la mama mzazi ni mahali patakatifu, ni tabernaklo ya binadamu mpya. Uhai wa binadamu mpya hukaa hapo kwa muda wote tangu kujipandikiza hadi kuzaliwa. Mama mwenye upendo hulitunza tumbo lake la uzazi dhidi ya uharibifu ili liwe mahali salama kwa mtoto wake. Ni mama tu mwenye kujua furaha na uchungu wa kuwa na mtoto tumboni mwake.
[Ndiyo maana watunzi wa nyimbo za dini hawakusita kulisia tumbo la mama kwa nyimbo mbalimbali. Hebu imba pamoja nami wimbo huu: “Heri tumbo la Bikira Maria”. Naye mwanzishaji anaimba: “Heri tumbo la Bikira Maria … na maziwa uliyonyonya”. Hapa unaona kuwa mtunzi huyu hasifii ‘tumbo’ tu, bali anasifia pia maziwa ya mama ambayo sote tulipata bahati ya kuyanyonya]
Tunaalikwa kuliheshimu, kulitunza na kulilinda tumbo la mama. Mtoto hujenga ushirika na mshikamano wa pekee na wa dhati kwa mama kwa njia ya tumbo la uzazi na maziwa anyonyayo. Ndani ya maziwa vimo virutubisho vyote vinavyohitajika kwa afya na kukua kwa mtoto.
5. Kutungwa mimba hadi kuzaliwa
Tangu kutungwa mimba hadi kuzaliwa binadamu anakuwa kimwili, kivionjo na kiakili. Ndiyo maana kila mwezi unaopita binadamu huyu mdogo anapitia mabadiliko kadhaa ambayo yanaonekana kwa namna mbalimbali. Hebu tuangalie mabadiliko hayo katika hatua za kukua mtoto kabla ya kuzaliwa hadi kuzaliwa. [picha za kukua mtoto hadi kuzaliwa].
6. Tunapohitimisha mada hii, tunaelewa kwa uhakika kuwa: