1. Maana Lunelle : ni dawa yenye mchanganyiko wa chachu bandia ya projestorene na estrogen ambayo mwanamke hudungwa kila baada ya mwezi na inaaminika kuzuia mimba kwa mwezi mmoja. Sindano ya Lunelle ina kiwango cha kuaminika cha kuzuia binadamu wapya kuzaliwa kiasi cha asilimia 99%
2. Utendaji wake
Inabadilisha ute kuwa mzito na kuzuia kupenya kwa urahisi kuelekea tumbo la uzazi na mirija yake
Pia sindano hii inaharibu ngozi nyororo ya tumbo la uzazi na kulifanya kushindwa kumpokea mtoto
Huzuia utoaji hormoni zinazohitajika kwa ajili ya kuivisha yai.
3. Madhara yake
Kutoka damu bila mpangilio, kutoka damu kwa muda mrefu au mfupi, kutoka damu kwa muda mrefu au mfupi nzito au nyepesi.
Kutopata hedhi kabisa
Kuumwa kichwa
Kuungezeka uzito kilo 2 kwa miezi 13
Matiti kuuma
Kuwa na wasiwasi
4. Wanawake wenye matatizo hayo wasitumie
Mjamzito
Matatizo ya ini
Kipanda uso (kichwa kuuma)
Matatizo ya moyo
Chanzo cha habari
Brian Clowes, Ph,D, ‘‘The Fact of Life ‘‘H.L.I (1997)
David A. Grime ; MD ; et al (edit)
‘‘Modern Contraception : Updates from the
Contraceptive Report (1997).
Robert A. Hatcher, MD ; MPH, et al
‘‘The Essentials of Contraceptive Technology :
A Handbook
For clinic staff (1997)’’