UTANGULIZI
Kwa miaka yote sisi wanawake wa Tanzania tumekabiliwa na madhara yatokanayo na matumizi ya vidhibiti mimba pamoja na utoaji wa mimba. Wahamasishaji wa uzazi wa mpango kwa njia za kisasa wametueleza muda wote kuwa njia za uzazi wa mpango hazina madhara na kwamba pia zinasaidia kuzuia kupata baadhi ya magonjwa, kama vile saratani ya tumbo la kizazi na ya kokwa. Tunapohudhuria huduma za kliniki wahudumu wa afya wanatushawishi kutumia dawa za uzazi wa mpango ili kuepuka kuzaa katika muda mfupi mfupi. Na kwa sasa hivi serikali na mashirika ya hiari ya ndani na njeyanaendesha kampeni kubwa ya kutumia uzazi wa mpango. Watu mashuhuri wanatumika katika kampeni hii. Wapo wana-muziki wa kisasa, waimbaji wa nyimbo za Injili, wapo wafanya kazi na wengine wengi. Katika kampeni hii tunaaminishwa kuwa njia za uzazi wa mpango hazina madhara na zinafaa hata kwa wasichana. Rasimu ya “Uzazi Salama” iliyoandaliwa na kufadhiliwa kwa kiasi kikubwa na mashirika ya nje, nayo imetumia kurasa nyingi kuitaka serikali kutunga sheria ya kuwalazimisha wanawake watumie njia za kisasa za uzazi wa mpango.
Sisi wanawake wa Tanzania, ambao ndio watumiaji wa njia hizo za uzazi wa mpango kwa njia za kisasa tunapenda kueleza masikitikio yetu kuwa, badala ya faida tunazoahidiwa, njia hizo za uzazi wa mpango zimetuletea simanzi kubwa. Wengi wetu tumeathirika kwa namna moja au nyingine; baadhi yetu wamepoteza maisha kwa kukosa huduma baada ya kupata madhara makubwa yatokanayo na njia hizo. Wahudumu wa afya hawatuambii ukweli kuhusu uwezekano wa kupata madhara baada ya kutumia njia hizo. Badala yake tukipata madhara, tunaporudi kuwajulisha tunaambiwa ni maudhi madogo madogo tu na yatakwisha baada ya muda mfupi. Wengine wanatushauri kubadilisha njia, yaani kama tulitumia vidonge vya majira, tunashauriwa kutumia sindano ya depo provera. Kwa mtindo huo baadhi yetu tumejikuta tukitumia njia zote – vidonge, sindano ya depo provera, vipandikizi, vitanzi bila mafanikio. Badala yake tumeshuhudia madhara yakiongezeka kila tunapobadilisha njia ya uzazi wa mpango. Wahamasishaji wanatulaghai kwa matangazo mazuri bila kusema ukweli wote juu ya njia za uzazi wa mpango.
Sasa tunasema tumechoka. Tumetendewa kama vyombo vya majaribio. Kwa maumivu yetu tumeendela kuvinufaisha viwanda vinavyotengeneza madawa hayo; tumeendelea kuwaneemesha wahamasishaji na wauzaji. Tumefanywa vyombo vya starehe katika masuala ya ngono kiasi kwamba badala ya kutukomboa, tumeendelea kudhalilishwa. Katika hatua hii tunasema basi, hatuwezi kuendelea kuteseka kwa faida ya wengine.
Na sasa tunaazimia kuanzisha shirika litakalowajumuisha wanawake wote waliotumia vidhibiti mimba na ambao wamedhurika kutokana na vidhibiti mimba hivyo. Tunataka kuliambia taifa kuwa HATUTANYAMAZA KAMWE. Hatutaki kutumiwa tena kama vyombo vya biashara. Hasara tunazozipata kwa madhara tunayoyapata zinatufanya kuendelea kuwa maskini na wanyonge katika nchi yetu. Tunashindwa kuchangia vema katika pato la familia zetu na taifa letu kwa sababu muda mwingi sisi tunakuwa wagonjwa.
Tunashangaa viongozi wa taifa letu wanapuuzia njia zinazofaa kwa wanawake kutumia ili kuweka mpishano wa uzao, kama vile njia za maumbile au za asili. Njia hizi ambazo mabibi zetu walizitumia na kuzienzi katika miaka yao, leo hii zimetupwa kando kama vile hazifai kwa lolote. Bibi zetu walitumia njia hizi wakajihakikishia afya zao, wakawazaa wazazi wetu na wameendelea kuwa na afya njema hadi uzeeni. Wameishi miaka mingi wakitoa mchango mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu. Njia hizi ambazo hazina madhara yoyote na zinaimairisha familia zetu, ndizo zinazopaswa kuhimizwa na viongozi wetu wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Katika shirika hili tunataka kuwajumuisha wenzetu waliotoa mimba kutokana na sababu mbalimbali. Tunataka nao washiriki katika jitihada zetu za kusema ukweli kwa uwazi, bila kufumbia macho madhara waliyoyapata kutokana na kujiingiza katika vitendo vya utoaji mimba. Vitendo vya utoaji mimba, licha ya kuleta madhara ya kimwili na kisaikolojia kwa wanawake, pia vimeleta vifo kwa baadhi ya wanawake ama kutokana na utoaji mimba mbaya, au kutokana na kutoka damu nyingi baada ya kutoa mimba. Baadhi ya wanawake wamebaki na ulemavu wa maisha. Licha ya hayo utoaji mimba husababisha taifa letu kupungukiwa na nguvu kazi, hata wataalamu na hata kupungua kwa idadi ya watu.
NA MAKAO MAKUU NA ANUANI:
Jina la lishirika litakuwa: “HATUTANYAMAZA KAMWE”
Makao makuu: yatakuwa Dar es Salaam
Anuani: hadi itakavyohitajika vinginevyo anuani yake itakuwa, S.L.P. 42749, Dar es Salaam
Katika kufikia malengo yake, Shirika litatumia njia zifuatazo katika kufikisha ujumbe
Fedha za shirika zitapatikana kwa njia za: